“Show me someone sick and happy, in danger and happy, dying and happy, exiled and happy, disgraced and happy. Show me! By God, how much I’d like to see a Stoic. But since you can’t show me someone that perfectly formed, at least show me someone actively forming themselves so, inclined in this way. . . . Show me!”
—EPICTETUS, DISCOURSES, 2.19.24–25a, 28

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari WEWE NI KAZI INAYOENDELEA…
Hakuna mtu ambaye amekamilika,
Pamoja na misingi tunayojiwekea ya kuyaishi maisha yetu, bado kuna nyakati tunaenda nje ya misingi hiyo.
Pamoja na malengo na mipango mizuri tunayokuwa tumejiwekea, kuna wakati tunafanya nje ya mipango hiyo.
Licha ya kuwa na ratiba ya kuendesha siku zetu, tukiwa na orodha ya mambo muhimu kufanya, bado kuna wakati tutafanya mambo ambayo hayakuwa kwenye ratiba au orodha ya vitu vya kufanya.

Unapojikuta kwenye hali kama hizi, pale ambapo umekwenda tofauti na ulivyopanga au kutarajia, usiumie sana nw kujiona hufai.
Badala yake jikumbushe kwamba wewe ni kazi inayoendelea, hujakamilika. Na hutakuja kukamilika mpaka siku unaondoka hapa duniani.
Kila siku ni nafasi ya wewe kujifunza na kupiga hatua zaidi.
Unaposhindwa kufuata kile ulichopanga au unachosimamia haimaanishi kwamba wewe ni dhaifu au ni mnafiki au haina haja ya kuwa na misingi au mipango.
Bali inamaanisha kwamba wewe ni kazi inayoendelea, na mapungufu yako yanakuonesha ni maeneo gani ambayo bado unahitaji kazi zaidi.

Wewe ni kazi inayoendelea, hakuna mtu anayekosoa jengo ambalo bado ujenzi unaendelea, kwa sababu bado ipo nafasi ya kufanya marekebisho.
Hivyo muhimu kwako ni kutambua yale maeneo ambayo una mapungufu na kuweza kuyafanyia kazi ili kuwa bora zaidi.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuendelea kujitengeneza na kuwa mtu bora kulingana na misingi unayoiishi na malengo na mipango yako.
#WeweNiKaziInayoendelea, #HakunaAliyekamilika, #KilaSikuMpyaNiFursaYaKuwaMtuMpya

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha