“That’s why the philosophers warn us not to be satisfied with mere learning, but to add practice and then training. For as time passes we forget what we learned and end up doing the opposite, and hold opinions the opposite of what we should.”
—EPICTETUS, DISCOURSES, 2.9.13–14
Ni siku nyingine nzuri, siku bora na ya kipekee sana kwetu.
Tuna nafasi hii bora sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari JIFUNZE, CHUKUA HATUA, FUNDISHA…
Kujifunza kitu kwa kusoma, kuangalia au kusikiliza peke yake haina msaada mkubwa kwako.
Utasahau haraka sana kile ambacho umejifunza.
Ukijifunza kitu, kisha ukakifanyia kazi kinakaa ma wewe muda mrefu, kinakuwa sehemu ya maisha yako.
Ukijifunza kitu, ukakifanyia kazi halafu ukawafundisha wengine pia, hapo unakuwa umekielewa kwa undani na unakuwa bora sana kwenye kitu hicho.
Hivyo hii ndiyo misingi kitatu muhimu sana unayopaswa kuiishi kila siku kwenye maisha yako.
Chochote unachojifunza hakikisha unakifanyia kazi na pia unawafundisha watu wengine.
Mtu mmoja amewahi kusema kujifunza halafu usichukue hatua ni kupoteza muda wako.
Na mwingine akasema, kama huwezi kumfundisha mtu kitu ulichojifunza basi wewe mwenyewe hujakijua vizuri.
JIFUNZE, CHUKUA HATUA, FUNDISHA, ni mchakato rahisi sana lakini ambao utaleta mapinduzi makubwa sana kwenye maisha yako.
Maana unaoochukua hatua, lazima ubadilike wewe mwenyewe.
Na unapowafundisha wengine, lazima kile unachofundisha kiwe sehemu ya maisha yako.
Ukawe na siku bora sana ya leo rafiki, siku ya KUJIFUNZA, KUCHUKUA HATUA NA KUFUNDISHA.
#JifunzeKilaSiku, #WekaKwenyeMatendo, #WafundisheWengine
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/kocha