“If then it’s not that the things you pursue or avoid are coming at you, but rather that you in a sense are seeking them out, at least try to keep your judgment of them steady, and they too will remain calm and you won’t be seen chasing after or fleeing from them.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 11.11
Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ambayo tumeiona leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari JIJENGEE UTULIVU…
Utulivu ni muhimu sana kwenye maisha,
Na utulivu unautengeneza mwenyewe kwa jinsi unavyoyachukulia mambo.
Mambo mengi unayoyakwepa kwenye maisha ndiyo unazidi kuyakaribisha kwako.
Chochote unachojaribu kukipinga au kushindana nacho unakikuza zaidi.
Hivyo kama kuna kitu hukitaki kwenye maisha yako, basi njia bora ni kujijengea utulivu, kwa kukipuuza.
Unapokuwa na utulivu wa ndani mambo ya nje yanatulia yenyewe.
Na pia utulivu unaambukizwa, unapokuwa na utulivu hata wale wanaokuzunguka wanakuwa na utulivu pia.
Pale kitu ambacho hukitegemea kimetokea, pale unapokutana na ugumu au changamoto kubwa, hatua ya kwanza jijengee utulivu.
Kwa kujijengea utulivu kwenye hali hizo, utaepuka kufanya mambo kuwa mabaya zaidi na utaweza kupata matokeo bora sana.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kujijengea utulivu kwa kila unachopitia.
JijengeeUtulivu, #UtulivuUnaambukizwa #UsifanyeMamboKuwaMagumuZaidi
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1