Habari rafiki yangu mpendwa,

Nimekuwa nakupa taarifa za semina yetu ya pili ya mwaka huu 2019 ambayo itaendeshwa kwa njia ya mtandao.

Hii ni semina ambayo inakwenda kutupa maarifa na hatua za kuchukua ili kuweza kutengeneza mfumo utakaotuwezesha kuendesha biashara zetu vizuri na kwa uhuru zaidi.

Kwa kuwa na mfumo, unaacha kumilikiwa na biashara na unaanza kuimiliki biashara yako. Biashara yako inaacha kukutegemea wewe kwa kila kitu na kuanza kutegemea mfumo, kitu ambacho kitakupa wewe uhuru mkubwa.

chati

Pia nilikupa njia mbili za kushiriki semina hii,

Njia ya kwanza ni uwe mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, kwa kulipa ada ya mwaka ambayo ni tsh laki moja.

Njia ya pili ni kujiunga na kundi maalumu la semina hii, kwa kulipa ada ya kushiriki semina pekee ambayo ni tsh elfu 20.

Napenda kuchukua nafasi hii kukujulisha kwamba kutakuwa na mabadiliko makubwa kwenye ushiriki wa semina hii.

Kwa mabadiliko haya, utaweza kushiriki semina kwa kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA pekee.

Hii ina maana kwamba ile nafasi ya kushiriki kwa kundi maalumu haipo tena.

Nitangulize kuomba radhi kwa sababu najua hili litaleta mtafaruku kwa wengi, kwa sababu wapo wengi ambao tayari walishajiunga na kundi hilo maalumu.

Sababu kubwa ya kubadili mfumo wa ushiriki ni wakati naandaa masoko ya semina hii nimeona jinsi yalivyo mazito na yanayohitaji umakini mkubwa kwenye kufundisha na hata kujibu maswali ya watu kuhusiana na mfumo. Na kuona itakuwa vigumu kwangu kuweza kuhudumia makundi mawili kwa masomo haya ambayo ni ya juu sana.

Hivyo nakwenda kuweka nguvu zangu zote kwenye kundi moja tu la KISIMA CHA MAARIFA, ili kuhakikisha wachache wanaopata maarifa haya yanaleta mabadiliko makubwa kwenye maisha yao na waweze kunufaika sana.

Kama unataka kushiriki semina hii ya kutengeneza MFUMO WA BIASHARA ambayo taarifa zake nitakupa hapo chini, basi jipange sasa na ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA.

Unajiunga na KISIMA CHA MAARIFA kwa kulipa ada ya mwaka ambayo ni tsh laki moja (100,000/=). Ukilipa ada hiyo unajifunza kwa mwaka mzima, ikiwepo kushiriki semina mbili zinazoendeshwa kwa njia ya mtandao na semina moja ya kukutana ana kwa ana.

Faida nyingine za kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA ni kila siku unaanza na tafakari ambayo inakuweka kwenye fikra sahihi za kuianza siku yako.

Pia kila juma kunakuwa na darasa la kujifunza mambo mbalimbali kuhusu mafanikio na pia kupata hamasa kutoka kwa wanamafanikio wengine.

Lakini pia ipo faida kubwa nyingine ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA ambayo ni kupata nafasi ya kujiunga kwenye KLABU ZA KISIMA CHA MAARIFA ambapo unakutana na wanamafanikio wenzako walio kwenye mkoa unaoishi, na kwa pamoja mnatengeneza timu ya mafanikio.

Karibu sasa ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA, uweze kupata maarifa haya bora sana yatakayokuwezesha kufanikiwa zaidi.

KARIBU KWENYE SEMINA YA MFUMO WA KUENDESHA BIASHARA YENYE MAFANIKIO.

Rafiki, baada ya kuona changamoto kubwa ambazo wafanyabiashara wengi wanapitia, hasa ya kukosa uhuru licha ya kuwa kwenye biashara. Na baada ya kujifunza na kutafiti kwa kina, nimekuandalia semina nzuri ya MFUMO WA KUENDESHA BIASHARA YENYE MAFANIKIO.

Semina hii itaendeshwa kwa njia ya mtandao wa wasap, hivyo utaweza kushiriki semina hii ukiwa popote duniani, na huhitaji kusafiri au kuacha shughuli zako za kila siku, ni kutenga tu muda ndani ya siku yako wa kufuatilia masomo ya semina.

Semina hii itaendeshwa kwa siku kumi, ambapo kila siku utapata somo la jinsi ya kutengeneza mfumo kwenye biashara yako. Masomo haya yatakuwa na mifano halisi ya hatua unazopaswa kuchukua ili biashara yako ijiendeshe kwa mfumo. Pia utapata nafasi ya kuuliza maswali na kupata ufafanuzi zaidi kwenye maeneo ambayo hayajaeleweka.

Semina hii itaanza rasmi tarehe 04/07/2019 mpaka tarehe 14/07/2019, kila siku asubuhi utapata somo la semina na utaweza kuuliza maswali kuhusiana na somo hilo. Masomo yote yatatumwa kwenye kundi la wasap na hivyo utaweza kuyafuatilia kwa urahisi.

Japokuwa semina hii inafanyika kwa njia ya mtandao, utajifunza kwa kina sana na kuondoka na mengi ya kwenda kufanyia kazi kuliko unavyoweza kujifunza kwenye semina ya kuhudhuria ana kwa ana. Kwa sababu semina hii ya mtandaoni inakwenda kwa kina sana kitu ambacho siyo rahisi kukifanya kwenye semina ya siku moja ya ana kwa ana.

JINSI YA KUSHIRIKI SEMINA YA MFUMO WA KUENDESHA BIASHARA.

Rafiki, ili uweze kushiriki semina hii nzuri sana itakayokupa uhuru kamili wa maisha yako, unapaswa kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA. Semina hii itaendeshwa moja kwa moja kupitia kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA.

KISIMA CHA MAARIFA ni moja ya programu za mafunzo na ukocha ninayoendesha, ambapo watu wanajifunza na kuhamasika kila siku, kisha kuchukua hatua na maisha yao kuwa bora sana.

Kama tayari wewe ni mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA na ada yako iko hai basi tayari umeshajihakikishia kushiriki semina hii. Wewe jiandae tu, kaa mkao wa kujifunza na utaondoka na nondo za kwenda kuiendesha biashara yako vizuri.

Kama ni mwanachama lakini ada yako inaisha karibuni, lipa ada yako mapema ili usikose nafasi ya kushiriki semina hii. Hakikisha hutoki ndani ya KISIMA CHA MAARIFA ili uweze kunufaika zaidi na mafunzo haya na mengine mengi.

Kama wewe siyo mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA na ungependa kushiriki semina hii ya MFUMO WA KUENDESHA BIASHARA YENYE MAFANIKIO, unapaswa kujiunga na kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA.

Hapa unalipa ada ya mwaka ambayo ni tsh laki moja (100,000/=). Kwa kulipa ada hiyo unapata nafasi ya kuwa ndani ya KISIMA CHA MAARIFA kwa mwaka mzima tangu tarehe uliyolipia. Utapata mafunzo ya semina mbili zinazofanyika mtandaoni kwa mwaka, na pia utapata nafasi ya kuwa karibu na mimi kocha wako, tukijifunza kwa kina. Pia tunakwenda kuwa ka Klabu za KISIMA CHA MAARIFA ambazo zinakupa jumuiya ya watu ulionao karibu ambao wanapiga hatua kufanikiwa zaidi.

JINSI YA KULIPA ADA.

Ili kulipa ada ya kushiriki semina hii, tuma kwenye namba zifuatazo;

TIGO PESA / AIRTEL MONEY – 0717 396 253 (Jina AMANI MAKIRITA)

M-PESA – 0755 953 887 (Jina AMANI MAKIRITA)

Ukishatuma ada, tuma ujumbe kwa wasap  kwenda namba 0717396253 wenye majina yako na maelezo kwamba umelipia KISIMA CHA MAARIFA.

MWISHO WA KULIPIA ILI KUSHIRIKI SEMINA.

Rafiki, mwisho wa kulipia ada yako ya KISIMA CHA MAARIFA ili uweze kupata mafunzo ya semina hii ni tarehe 01/07/2019.

Ili ujihakikishie kushiriki semina hii na kuweza kuikuza biashara yako, lipa ada yako mapema kabla ya tarehe hiyo ya mwisho.

Ninaamini unapenda sana kupiga hatua na kufanikiwa kwenye biashara yako,

Ninaamini hilo linawezekana kabisa, kwa sababu nimeona wengi wakianzia chini na kupiga hatua zaidi.

Na nina imani kubwa kwenye mafunzo niliyokuandalia, yanakwenda kukupa uhuru mkubwa sana kwenye maisha yako, hata kama biashara yako ni ndogo sana.

Karibu sana ushiriki semina hii ya MFUMO WA BIASHARA na utaweza kupiga hatua zaidi. Kumbuka kulipa ada yako kwa wakati, kabla ya tarehe 01/07/2019 ili uweze kunufaika na mafunzo haya yatakayoiwezesha biashara yako kukua zaidi.

Nakusubiri kwa shauku kubwa kwenye semina hii ya MFUMO WA BIASHARA, kwa sababu najua utaondoka na mengi ya kuiwezesha biashara yako kukua zaidi. Usipange kukosa semina hii.

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali. Kupata Huduma Za Ukocha Tembelea; www.amkamtanzania.com/kocha

Kupokea makala moja kwa moja kwenye email yako fungua hapa na ujaze fomu; https://amkamtanzania.com/jiunge