“When you’ve done well and another has benefited by it, why like a fool do you look for a third thing on top—credit for the good deed or a favor in return?”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 7.73

Asubuhi njema wanamafanikio wote,
Hongereni sana wote kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo,
Ni nafasi bora sana na ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari KUFANYA KILICHO SAHIHI INATOSHA…
Watu wengi wamekuwa wanafanya kilicho sahihi kama maigizo,
Wanafanya kilicho sahihi ili waonekane wamefanya,
Au wanafanya ili wasifiwe au kulipwa fadhila.
Lakini hiyo siyo sababu sahihi ya kufanya kilicho sahihi.

Sababu sahihi ya kufanya kilicho sahihi ni kwa sababu ndiyo kitu sahihi kufanya.
Fanya kitu kilicho sahihi, kwa sababu ndiyo kitu sahihi kwako kufanya.
Siyo kwa sababu unayaka uonekane,
Wala kwa sababu unataka usifiwe,
Au kutaka wengine nao wakufanyie kitu fulani.

Wewe fanya kile kilicho sahihi mara zote, kwa sababu ndiyo kitu sahihi kwako kufanya.
Na ukiishi kwa msingi huu utakuwa mtu bora sana, mara zote utafanya yaliyo sahihi, bila ya kujali kama kuna mtu anaangalia au la, kama kuna mtu anakulipa au la.

Ubinadamu ni kufanya kile kilicho sahihi mara zote.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kufanya kile kilicho sahihi mara zote. Usijali nani anaangalia au unalipwa nini. Wewe fanya kilicho sahihi. Inatosha.
#FanyaKilichoSahihi #UsiigizeMaisha #IshiMaishaYakoLeo

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1