“How disgraceful is the lawyer whose dying breath passes while at court, at an advanced age, pleading for unknown litigants and still seeking the approval of ignorant spectators.”
—SENECA, ON THE BREVITY OF LIFE, 20.2

Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari KAZI YAKO SIYO ADHABU YA KIFO…
Kazi au biashara unayoifanya siyo adhabu ya kifo, kwamba inabidi uifanye mpaka siku unayokufa.
Bali ni kitu ambacho unapaswa kufanya pale unapokuwa na msukumo wa kufanya kutoka ndani yako, unapokuwa unapenda na kufurahia kufanya.

Unapofika wakati ambao hutaki au huwezi kufanya tena, uwe tayari kuachana na kazi au biashara hiyo na kufanya mambo mengine.
Watu wengi wamekuwa wanapoteza maisha na miaka yao kwa kufanya kazi au biashara ambazo hawazipendi na pia haziwapi yake maisha wanayotaka.
Lakini wanajiambia inabidi waendelee kufanya kwa sababu hawana namna.

Rafiki wewe una namna,
Una uhuru mkubwa wa kuchagua ni nini ufanye na nini usifanye.
Tupo kwenye zama ambazo kila mtu ana uhuru mkubwa wa kuchagua jinsi atakavyoyaendesha maisha yake, usipoteze nafasi hii.

Kama kazi au biashara unafurahia kuifanya na inakupa kile unachotaka, unaweza kuifanya kwa maisha yako yote.
Lakini kama kazi au biashara huifurahii na wala haikupi unachotaka, unaweza kuacha kuifanya, siyo adhabu ya kifo kwamba lazima uitumikie maisha yako yote.

Upo huru, chagua maisha unayotaka, chagua kazi au biashara yenye maana kwako.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuendesha maisha yako kwa uhuru, kwa kuchagua kufanya kazi au biashara unayoipenda. Na kama kazi au biashara unayofanya sasa huipendi, kumbuka hiyo siyo adhabu ya kifo, weka sasa mipango ya kuondoka hapo na ifanyie kazi ili uweze kuwa huru.
#KaziSiyoAdhabuYaKifo #FanyaUnachopenda #MaishaNdiyoHaya

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1