“Apply yourself to thinking through difficulties—hard times can be softened, tight squeezes widened, and heavy loads made lighter for those who can apply the right pressure.”
—SENECA, ON TRANQUILITY OF MIND, 10.4b
Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari UNA NAFASI YA KUWA BORA ZAIDI…
Haijalishi unapitia magumu kiasi gani,
Haijalishi mambo yamekwama kiasi gani,
Haijalishi umejaribu mara ngapi na ukashindwa,
Bado ipo nafasi ya wewe kuwa bora zaidi.
Una nafasi ya kuwa bora zaidi ya ulivyo sasa,
Una nafasi ya kupiga hatua zaidi ya ulizopiga sasa,
Hakuna kitu chochote cha nje kinachoweza kukuzuia, kama maamuzi ya ndani yatakuwa imara na unayoyasimamia.
Nyakati ngumu zinaweza kulainishwa,
Mizigo mizito inaweza kufanywa myepesi,
Mambo magumu yanaweza kufanywa rahisi,
Kama tu utatumia akili yako vizuri na kuweka juhudi sahihi.
Una nafasi ya kuwa bora zaidi bila ya kujali umekwama wapi sasa. Itumie nafasi hiyo kwenye kila hali.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kutumia akili yako vizuri ili kuweza kuvuka kila aina ya ugumu unaopitia kwenye maisha yako.
#HakunaLisilowezekana #KunaNafasiYaKuwaBoraZaidi #UsikateTamaa
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1