“This can be swiftly taught in very few words: virtue is the only good; there is no certain good without virtue; and virtue resides in our nobler part, which is the rational one. And what can this virtue be? True and steadfast judgment. For from this will arise every mental impulse, and by it every appearance that spurs our impulses will be rendered clear.”
—SENECA, MORAL LETTERS, 71.32
Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo,
Ni siku mpya na ya kipekee sana kwetu ambapo tumepata nafasi nyingine nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU , UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.
Asubuhi ya leo tutafakari MAHAKAMA KUU YA AKILI…
Mahakama kuu ya akili yako ni kutenda mema,
Kitu sahihi kwako wewe kufanya ni kuwa mwema na kufanya yake yaliyo mema.
Kama kitu siyo chema, siyo sahihi kwako kufanya.
Akili zetu zinajua kabisa kipi sahihi na kipi siyo sahihi kufanya.
Hivyo hata kama utachagua kufanya kisicho sahihi, kwa kuwadanganya watu wa nje kwamba ni sahihi, bado hutaweza kuidanganya akili yako.
Na hilo litakusumbua sana kwa sababu ndani ya nafsi yako utajua hujasimamia kilicho sahihi.
Chagua sasa kuishi maisha ambayo hayana majuto, kwa kuchagua kufanya kile kilicho sahihi wakati wote.
Kuwa mtu mwema wakati wote,
Siyo kwa sababu wengine wanaona au kwa sababu unataka uonekane kwa namna fulani,
Bali kwa sababu ndiyo ulichochagua kufanya.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuwa mwema na kufanya kilicho sahihi kwa sababu mahakama yako kuu (AKILI) haidanganywi.
#KuwaMwema #FanyaKilichoSahihi #HuweziKujidanganyaMwenyewe
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1