Rafiki yangu mpendwa, kwenye makala hii utakwenda kujifunza kwa nini unakwama kwenye mafanikio na njia moja ya uhakika ya kukutoa hapo ulipokwama sasa. Karibu twende pamoja.
Kila mtu kwenye maisha huwa anafika hatua fulani na kukwama.
Mtu unaanzia chini kabisa, unaweka juhudi kubwa, unapiga hatua fulani kubwa mwanzoni, ambazo zinakupa hamasa na matumaini makubwa.
Lakini baada ya kuanza kupata mafanikio kidogo, ukuaji unasimama. Kila unapojaribu kuweka juhudi zaidi hakuna matokeo bora unayopata, matokeo yanakuwa yale yale na wakati mwingine yanapungua zaidi.
Hapa ndipo watu wengi hukata tamaa na kushindwa kupiga hatua zaidi, wengi huona kama wameshafika ukomo wa mafanikio na hakuna hatua wanayoweza kupiga tena.
Rafiki, ukweli ni kwamba hakuna ukomo wa mafanikio, unaweza kuendelea kupiga hatua kadiri utakavyo bila ya kujali umefika juu kiasi gani.
Lakini kuna tatizo moja kubwa ambalo huwa linajitokeza pale unapoanza kupiga hatua, ambalo huwa ni mazoea na kuona umeshajua kila unachopaswa kufanya.
Mwanasayansi Einstein amewahi kunukuliwa akisema huwezi kutatua tatizo jipya kwa fikra zile zile ambazo zimetengeneza tatizo hilo. Inabidi uwe na fikra za juu zaidi ya zile zilizotengeneza tatizo ili uweze kulitatua. Kwa upande wa mafanikio inamaanisha kwamba huwezi kutatua mkwamo uliofikia kimafanikio kwa kuendelea kufanya unachofanya sasa, unahitaji kubadilika wewe kwanza, kuwa wa juu zaidi ndiyo uweze kutoka hapo ulipokwama.
Mwandishi Marshall Goldsmith kwenye kitabu chake kinachoitwa What Got You Here Won’t Get You There, anasema kwamba kile ulichofanya ukafika hapo ulipo sasa, siyo kitakachokuwezesha kupiga hatua zaidi. Na hapa ndipo wengi wanapokwama kwenye safari ya mafanikio. Wanafanya kitu kimoja na kupata mafanikio kidogo na wanakariri hicho ndiyo sahihi, basi wanaendelea kufanya hicho hicho hata kama hakileti tena matokeo mapya.
Kwa mifano hiyo miwili, ipo wazi kwamba ili kutoka hapo ulipokwama sasa, unahitaji kuwa mtu tofauti kwanza, unahitaji kupiga kwanza hatua wewe binafsi kabla hujaweza kupiga hatua zaidi kwenye yale unayofanya.
Hatua unazopaswa kupiga wewe mwenyewe siyo hatua za kawaida, ni mabadiliko makubwa katika mfumo wako wa kufikiri na maisha kwa ujumla. Siyo hatua rahisi kufanya na ndiyo maana wengi huwa wanakwama kwenye mafanikio kidogo, wasiweze kupiga hatua zaidi.
Na hapa ndipo mimi kocha wako nimekuletea njia ya uhakika ya kukuwezesha wewe kupiga hatua na kutoka hapo ulipokwama sasa.
Njia hiyo ni programu ya GAME CHANGERS, ambapo programu hii inakupa manufaa mawili kwa wakati mmoja, ambayo yana nguvu ya kukuwezesha kubadilika kabisa. Nguvu ya kwanza ni kuwa na kocha ambaye anakuongoza kwa karibu. Na nguvu ya pili ni kuwa pamoja na watu ambao nao wanabadilika. Katika kufanikiwa, vitu hivi viwili vimedhibitishwa kuleta matokeo bora sana, kuwa na kocha na kuzungukwa na watu ambao nao wanataka kufanikiwa.
Kwenye programu hii ya GAME CHANGERS, nitafanya kazi kwa karibu na WATU WATANO tu kwa kipindi cha siku 30. Na ndani ya siku hizo 30 kutakuwa na mabadiliko makubwa sana, kila mtu atapata MPENYO wake wa ukuaji na baada ya siku hizo 30 mtu atatoka akiwa wa tofauti kabisa na ambaye ataweza kukua zaidi bila ya kujizuia yeye mwenyewe.
Kama kuna eneo lolote la maisha yako unaona umekwama, ambapo unajaribu kuweka juhudi sana lakini huoni matokeo ya tofauti, basi jua programu hii imekuja kwa ajili yako.
Kama ni kipato kimegoma kuongezeka kwa muda sasa, jua tatizo siyo kipato, bali tatizo ni wewe. Kama ni mahusiano yanakusumbua kwa muda sasa, jua tatizo linaanza na wewe. Na hata kama ni afya inakupa changamoto kwa muda, jua kuna namna ambayo fikra na tabia zako zinachangia hilo.
Karibu sana kwenye GAME CHANGERS ambayo utakwenda kutengeneza upya mfumo wa maisha yako, kuanzia fikra mpaka matendo, kitu ambacho kitakufungua sana. Kwenye programu hii utakwenda kuondoa kabisa breki ambazo unajiwekea wewe mwenyewe kwenye kupiga hatua zaidi.
UTARATIBU WA GAME CHANGERS.
Kwa kuingia kwenye programu hii ya GAME CHANGERS, utapata nafasi ya kufanya kazi moja kwa moja na Kocha Dr Makirita pamoja na watu wengine wanne katika kutoka pale ulipokwama.
Utapata nafasi ya kujadili ulipokwama kwa kina na Kocha, na kisha kwa pamoja mtaweka mkakati utakaofanyia kazi kwa siku 30.
Utawekwa kwenye kundi maalumu la wasap la programu hii ambapo huko utakuwa pamoja na wengine wanaofanyia kazi mabadiliko kwenye maisha yao.
Kila siku ya jumamosi, kuanzia saa 12 jioni kutakuwa na simu ya pamoja ya watu wote watano waliopo kwenye programu hii pamoja na kocha kwa ajili ya kupitia hatua ambazo kila mtu amepiga kwa juma zima. Katika simu hii ya pamoja, kila mtu anapata nafasi ya kumshauri mwenzake katika hatua anazochukua na changamoto anazokutana nazo.
Kila siku kwa siku 30 utapata somo moja la misingi ya GAME CHANGERS ambalo litakupa maarifa ya kupiga hatua zaidi kwenye maisha yako. Kwenye kila somo na kila msingi, kutakuwa na mafunzo au kitabu cha rejea ambapo utaweza kujifunza kwa kina zaidi.
Kwa siku zote 30 za programu hii, una uhuru wa kuwasiliana na kocha katika muda wowote, kuuliza chochote na kupatiwa majibu au ushauri wa kitu sahihi kufanya kwa pale ulipokwama.
Unaweza kushiriki programu hii ukiwa sehemu yoyote nchini Tanzania, na ambapo una mtandao wa simu na mtandao wa intaneti.
ADA YA GAME CHANGERS NA TAREHE YA KUANZA.
Ada ya kushiriki kwenye msimu huu wa GAME CHANGERS SEPTEMBA 2019 ni tsh laki tatu (300,000/=) kwa mwezi mzima, ambayo ni sawa na uwekezaji wa tsh elfu 10 kwa siku.
Kwa uwekezaji huu ambao unaonekana ni mkubwa, utaweza kupata thamani ambayo ni mara kumi ya ulichowekeza. Ninakuhakikishia kwamba kama utajitoa kweli kwenye programu hii, basi utaweza kupata thamani mara 10 ya uwekezaji huo. Yaani kwa kiwango cha chini sana, matokeo utakayopata thamani yake itakuwa shilingi milioni 3.
Programu hii ya GAME CHANGERS itaanza rasmi tarehe 01/09/2019.
Ili kupata nafasi ya kushiriki programu hii unapaswa kulipa ada ya ushiriki, tsh 300,000/=.
Nafasi za kushiriki programu hii ni 5 pekee. Na nafasi zinatolewa kwa wale wanaowahi. Yaani nafasi zikishajaa hakuna tena nyingine itakayopatikana.
Hivyo nikushauri sana uchukue hatua mara moja unapopata ujumbe huu ili usikose nafasi hii. Kwa sababu programu hii inakuja mara chache sana na huu ni msimu wa mwisho wa programu hii kwa mwaka huu 2019.
Mwisho wa kutuma ada ili kupata nafasi ya kushiriki programu hii ni tarehe 29/08/2019. Na kwa wale watakaokuwa wamepata nafasi, siku ya tarehe 30/08/2019 nitakuwa na maongezi ya simu na kila mmoja ili kujadili kwa kina alipokwama na kuweka mipango ya kufanyia kazi.
Tarehe 31/08/2019 tutaanza rasmi programu yetu na siku hiyo jioni saa 11 tutakuwa na maongezi ya simu ya kwanza kwa ajili ya kutambuana na kupeana mikakati ya kila mmoja wetu.
Karibu sana kwenye GAME CHANGERS, programu pekee inayoweza kukutoa hapo ulipokwama sasa.
Kama una nia ya kushiriki kwenye programu hii, tuma ujumbe sasa kwa njia ya wasap kwenda namba 0717396253 wenye maneno GAME CHANGERS ili kujiwekea nafasi.
Naamini hutaiacha nafasi hii adimu sana kwako kuondoka kwenye mkwamo ikupite. Chukua hatua sasa ili uweze kufanikiwa zaidi na kuondoka hapo ulipokwama sasa.
Tuma ujumbe sasa kwenye wasap namba 0717396253 kujiwekea nafasi ya SIKU 30 ZA KUONDOKA KWENYE MKWAMO NA KUKUA ZAIDI.
MUHIMU; Rafiki, nafasi za kushiriki programu hii ni 5 pekee, ni nafasi chache mno na hazitaongezwa, na hii ni nafasi ya mwisho unayoweza kupata ya kushiriki programu hii kwa mwaka huu 2019. Hivyo usikilize moyo wako, kama unakuambia hiki ni kitu unachohitaji basi unakihitaji kweli, usiendelee kujichelewesha kukua zaidi. Tuma ujumbe sasa kwa wasap namba 0717396253 kujiwekea nafasi ya kuwa kwenye programu hii ya GAME CHANGERS kwa msimu huu.
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,