“Just as the nature of rational things has given to each person their rational powers, so it also gives us this power—just as nature turns to its own purpose any obstacle or any opposition, sets its place in the destined order, and co-opts it, so every rational person can convert any obstacle into the raw material for their own purpose.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 8.35

Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana tuliyoiona leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Kwa msingi wetu wa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA pamoja na mwongozo wa AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA tunakwenda kufanya makubwa leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari KILA KITU KINA FAIDA KWAKO…
Hakuna kitu kinachotokea kwenye maisha yako, iwe kizuri au kibaya, ambacho hakina manufaa kwako.
Kila kitu kinachotokea au unachokutana nacho kwenye maisha, kina faida kwako.

Katika kila kikwazo unachokutana nacho ipo njia.
Katika kila ugumu unaokutana nao lipo somo la kujifunza.
Katika kila hali, tunapata tunachotaka au tunapata funzo muhimu kuhusu maisha na sisi wenyewe.

Hivyo rafiki, kwa kila hali unayokutana nayo, hasa hali ngumu au usiyotegemea, usione kama ndiyo mwisho wa safari yako,
Bali huo ndiyo wakati wa kujiuliza kuna faida gani kwenye hilo.
Na kwa hakika, kila hali, kila unachokutana nacho, kina faida na manufaa kwako kama utayaangalia na kuyatumia.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuona manufaa kwenye kila hali unayoipitia kwenye maisha yako, iwe ni nzuri au mbaya.
#KilaKituKinaFaida #KilaKikwazoKinaNjia #UsikateTamaaKwaUgumuUnaokutanaNao

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1