Rafiki yangu mpendwa, kwenye makala hii nakwenda kukuonesha jinsi ambavyo unaweza kuwekeza shilingi laki tatu na ndani ya siku 30 ukapata thamani ya milioni tatu. Karibu twende pamoja.

Rafiki, kama tumekuwa pamoja kwa muda sasa, unajua kabisa kuna uwekezaji mmoja ambao nimekuwa nakushauri sana uufanye. Huu ni uwekezaji ambao hakuna anayeweza kukuibia na wala hauathiriwi na kuyumba kwa uchumi. Uwekezaji huo huwa unaongezeka thamani kadiri unavyokwenda.

Uwekezaji ninaouzungumzia hapa, ni uwekezaji ndani ya mtu binafsi. Unapowekeza ndani yako mwenyewe, kwa kupata maarifa na miongozo sahihi, hakuna anayeweza kukuibia, hakuna anayeweza kukudhulumu na kadiri muda unavyokwenda, thamani ya uwekezaji wako inakua zaidi.

Uwekezaji huu unaufanya kwa kununua maarifa, kupitia vitabu na kozi mbalimbali, lakini pia kwa kulipia huduma za ukocha, ambapo unapata mwongozo na usimamizi wa karibu kwenye yale unayofanya.

Leo nakwenda kukushirikisha ushuhuda wa mtu ambaye uwekezaji binafsi umeweza kuwa na matokeo makubwa sana kwake kwa kipindi kifupi;

Habari yako Kocha?

Leo nilikuwa najifanyia tathmini ya hii programu ya GAME CHANGERS ambayo tumeimaliza jana, mwanzoni nilikuwa nina hofu ya kutoa tsh 300,000 na kuona kama vile naweza nisiambulie kitu.

kwa kipindi hiki kifupi matokeo niliyoyapata ni makubwa sana, kwanza kwa kipindi cha wiki mbili nimeweza kuongeza tsh 888,600, ambayo ni faida ya wiki mbili kwenye mfereji mpya wa biashara ya kuuza float ya M-pesa kwa mawakala.  Nimejifunza mengi sana kwa thamani kubwa sana uliyoweka kwenye programu hii.

Mwezi ujao nategemea kupata zaidi ya 3,000,000 kama ongezeko la faida kwenye biashara ambayo mwanzoni nilikuwa nafanya kwa mazoea sana. Unaweza kushangaa nawezaje kupata kiasi kikubwa cha fedha namna hii lakini kikubwa ni kuweka kazi tena kazi kweli kweli.

Kweli Kocha nimeamini kuwa bilionea inawawezeka cha muhimu zaidi ni kutumia uwezo wetu wa kufikiri na kufanya yale ambayo tu yanachangia kwenye kutimiza ndoto zetu.

Binafsi nakushukuru sana tena sana, Kocha nasema Asante sana. Mungu atujalie maisha marefu ili mwaka 2040 watanzania tushuhudie ukiapishwa na kuwa rais wa Tanzania. Kila la kheri  Kocha.

Leonard Amo

Ushuhuda GAME CHANGERS; Leonard Amo.jpg

Kama ulivyosoma kwenye ushuhuda wa mwenzetu Leonard hapo juu, uwekezaji ndani yako ninafsi unalipa sana, hasa pale unapowekeza kwenye huduma zinazokusukuma kuchukua hatua zaidi.

Nichukue nafasi hii kukumbusha kwamba programu maalumu ya ukocha ya GAME CHANGERS itakuwa na msimu wake wa mwisho mwezi septemba mwaka huu 2019. Ni programu yenye nguvu kubwa ya kukusukuma na kukuwajibisha kuchukua hatua na hivyo kutokubaki hapo ulipo sasa.

Hii ndiyo programu iliyomwezesha mwenzetu Leonard kuweza kutengeneza thamani zaidi ya milioni tatu kwa muda mfupi wa siku 30.

Kwenye programu hii ya GAME CHANGERS, unapata manufaa mawili kwa wakati mmoja, ambayo yana nguvu ya kukuwezesha kubadilika kabisa. Nguvu ya kwanza ni kuwa na kocha ambaye anakuongoza kwa karibu. Na nguvu ya pili ni kuwa pamoja na watu ambao nao wanabadilika. Katika kufanikiwa, vitu hivi viwili vimedhibitishwa kuleta matokeo bora sana, kuwa na kocha na kuzungukwa na watu ambao nao wanataka kufanikiwa.

Kwenye programu hii ya GAME CHANGERS, nitafanya kazi kwa karibu na WATU WATANO tu kwa kipindi cha siku 30. Na ndani ya siku hizo 30 kutakuwa na mabadiliko makubwa sana, kila mtu atapata MPENYO wake wa ukuaji na baada ya siku hizo 30 mtu atatoka akiwa wa tofauti kabisa na ambaye ataweza kukua zaidi bila ya kujizuia yeye mwenyewe.

Kama kuna eneo lolote la maisha yako unaona umekwama, ambapo unajaribu kuweka juhudi sana lakini huoni matokeo ya tofauti, basi jua programu hii imekuja kwa ajili yako.

Kama ni kipato kimegoma kuongezeka kwa muda sasa, jua tatizo siyo kipato, bali tatizo ni wewe. Kama ni mahusiano yanakusumbua kwa muda sasa, jua tatizo linaanza na wewe. Na hata kama ni afya inakupa changamoto kwa muda, jua kuna namna ambayo fikra na tabia zako zinachangia hilo.

Karibu sana kwenye GAME CHANGERS ambayo utakwenda kutengeneza upya mfumo wa maisha yako, kuanzia fikra mpaka matendo, kitu ambacho kitakufungua sana. Kwenye programu hii utakwenda kuondoa kabisa breki ambazo unajiwekea wewe mwenyewe kwenye kupiga hatua zaidi.

UTARATIBU WA GAME CHANGERS.

Kwa kuingia kwenye programu hii ya GAME CHANGERS, utapata nafasi ya kufanya kazi moja kwa moja na Kocha Dr Makirita pamoja na watu wengine wanne katika kutoka pale ulipokwama.

Utapata nafasi ya kujadili ulipokwama kwa kina na Kocha, na kisha kwa pamoja mtaweka mkakati utakaofanyia kazi kwa siku 30.

Utawekwa kwenye kundi maalumu la wasap la programu hii ambapo huko utakuwa pamoja na wengine wanaofanyia kazi mabadiliko kwenye maisha yao. Kundi hili litaendelea hata baada ya programu kumalizika.

Kila siku ya jumamosi, kuanzia saa 12 jioni kutakuwa na simu ya pamoja ya watu wote watano waliopo kwenye programu hii pamoja na kocha kwa ajili ya kupitia hatua ambazo kila mtu amepiga kwa juma zima. Katika simu hii ya pamoja, kila mtu anapata nafasi ya kumshauri mwenzake katika hatua anazochukua na changamoto anazokutana nazo.

Kila siku kwa siku 30 utapata somo moja la misingi ya GAME CHANGERS ambalo litakupa maarifa ya kupiga hatua zaidi kwenye maisha yako. Kwenye kila somo na kila msingi, kutakuwa na mafunzo au kitabu cha rejea ambapo utaweza kujifunza kwa kina zaidi.

Kwa siku zote 30 za programu hii, una uhuru wa kuwasiliana na kocha katika muda wowote, kuuliza chochote na kupatiwa majibu au ushauri wa kitu sahihi kufanya kwa pale ulipokwama.

Unaweza kushiriki programu hii ukiwa sehemu yoyote nchini Tanzania, na ambapo una mtandao wa simu na mtandao wa intaneti.

ADA YA GAME CHANGERS NA TAREHE YA KUANZA.

Ada ya kushiriki kwenye msimu huu wa GAME CHANGERS SEPTEMBA 2019 ni tsh laki tatu (300,000/=) kwa mwezi mzima, ambayo ni sawa na uwekezaji wa tsh elfu 10 kwa siku.

Kwa uwekezaji huu ambao unaonekana ni mkubwa, utaweza kupata thamani ambayo ni mara kumi ya ulichowekeza. Ninakuhakikishia kwamba kama utajitoa kweli kwenye programu hii, basi utaweza kupata thamani mara 10 ya uwekezaji huo. Yaani kwa kiwango cha chini sana, matokeo utakayopata thamani yake itakuwa shilingi milioni 3.

Programu hii ya GAME CHANGERS itaanza rasmi tarehe 01/09/2019.

Ili kupata nafasi ya kushiriki programu hii unapaswa kulipa ada ya ushiriki, tsh 300,000/=.

Nafasi za kushiriki programu hii ni 5 pekee. Na nafasi zinatolewa kwa wale wanaowahi. Yaani nafasi zikishajaa hakuna tena nyingine itakayopatikana.

Hivyo nikushauri sana uchukue hatua mara moja unapopata ujumbe huu ili usikose nafasi hii. Kwa sababu programu hii inakuja mara chache sana na huu ni msimu wa mwisho wa programu hii kwa mwaka huu 2019.

Mwisho wa kutuma ada ili kupata nafasi ya kushiriki programu hii ni tarehe 29/08/2019. Na kwa wale watakaokuwa wamepata nafasi, siku ya tarehe 30/08/2019 nitakuwa na maongezi ya simu na kila mmoja ili kujadili kwa kina alipokwama na kuweka mipango ya kufanyia kazi.

Tarehe 31/08/2019 tutaanza rasmi programu yetu na siku hiyo jioni saa 11 tutakuwa na maongezi ya simu ya kwanza kwa ajili ya kutambuana na kupeana mikakati ya kila mmoja wetu.

Karibu sana kwenye GAME CHANGERS, programu pekee inayoweza kukutoa hapo ulipokwama sasa.

Kama una nia ya kushiriki kwenye programu hii, tuma ujumbe sasa kwa njia ya wasap kwenda namba 0717396253 wenye maneno GAME CHANGERS ili kujiwekea nafasi.

Naamini hutaiacha nafasi hii adimu sana kwako kuondoka kwenye mkwamo ikupite. Chukua hatua sasa ili uweze kufanikiwa zaidi na kuondoka hapo ulipokwama sasa.

Tuma ujumbe sasa kwenye wasap namba 0717396253 kujiwekea nafasi ya SIKU 30 ZA KUONDOKA KWENYE MKWAMO NA KUKUA ZAIDI.

MUHIMU; Rafiki, nafasi za kushiriki programu hii ni 5 pekee, ni nafasi chache mno na hazitaongezwa, na hii ni nafasi ya mwisho unayoweza kupata ya kushiriki programu hii kwa mwaka huu 2019. Hivyo usikilize moyo wako, kama unakuambia hiki ni kitu unachohitaji basi unakihitaji kweli, usiendelee kujichelewesha kukua zaidi. Tuma ujumbe sasa kwa wasap namba 0717396253 kujiwekea nafasi ya kuwa kwenye programu hii ya GAME CHANGERS kwa msimu hii.

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,

Kocha Dr Makirita Amani,

www.amkamtanzania.com/kocha

PS; AHADI YANGU kwako wewe rafiki yangu ni hii, kwa kiwango cha chini kabisa, unakwenda kupata thamani ambayo ni mara kumi ya ada utakayolipa. Na kama hilo halitatokea basi utaniambia na nitakurejeshea ada uliyolipa. Kusudi langu la kwanza ni kukuona wewe unapiga hatua kabla mimi sijanufaika, hivyo kama hutanufaika, nikuhakikishie kwamba hutapoteza fedha yako. Tuma ujumbe sasa kwenye wasap namba 0717396253 ujiwekee nafasi yako ya kushiriki programu hii.