Watu huwa wanafanya maamuzi kwa hisia na siyo kwa kufikiri.
Hivyo kama kuna kitu unataka watu wafanye, basi gusa hisia zao kama unataka kuwashawishi wafanye.
Usitoe tu maelezo makavu ambayo yanaelezea kitu, bali toa maelezo yenye hisia ndani yake, ambayo yatamsukuma mtu kuchukua hatua sasa.
Hisia zenye ushawishi mkubwa kwa wengi ni hisia za hofu na tamaa.
Watu huwa wanahofia sana kupoteza kile walichonacho au kukosa kitu fulani kizuri. Hivyo unapowaonesha kwamba kuna kitu watapoteza kama hawatachukua hatua, wanasukumwa kuchukua hatua zaidi.
Kadhalika watu huwa wanapenda kupata vitu vizuri kwa urahisi na haraka. Kama utaweza kuwaeleza watu ni kipi kizuri wanakwenda kupata kwa urahisi na haraka, watasukumwa kuchukua hatua zaidi.
Iwe unauza au unataka kumshawishi mtu akubaliane na wewe kwenye jambo lolote lile, kugusa hisia zao kutakupa matokeo mazuri kuliko kutoa maelezo makavu ambayo hayagusi kabisa hisia.
Kama unataka majibu na matokeo mazuri, gusa hisia za wengine.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
Ahsante kocha hz ni mbinu nzuri sana katika kushawish na kuuza …….
LikeLike
Karibu
LikeLike