“Therefore, explain why a wise person shouldn’t get drunk—not with words, but by the facts of its ugliness and offensiveness. It’s most easy to prove that so-called pleasures, when they go beyond proper measure, are but punishments.”
—SENECA, MORAL LETTERS, 83.27

Ni siku mpya, siku bora na ya kipekee wana kwetu.
Tumeiona nafasi hii nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA.
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA.
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa vitu hivi vitatu, tunayo nafasi ya kufanya makubwa sana leo na kila siku ya maisha yetu.

Asubuhi ya leo tutafakari TUMIA MANUFAA KUSHAWISHI…
Kama unataka kuwashawishi watu kuchukua hatua fulani, gusa manufaa yao binafsi kwenye kitu hicho.
Waoneshe ni nini wanakwenda kunufaika nacho wanapochukua hatua,
Au nini wanakwenda kukosa wasipochukua hatua.

Kwa asili sisi binadamu ni wabinafsi, huwa tunajali zaidi mambo yetu binafsi kuliko mambo ya wengine.
Hivyo kitu kinapokuwa na manufaa kwetu, huwa tunasukumwa kukifanya.
Katumie nguvu hiyo kwa wengine na utaona jinsi wanavyoshawishika kuchukua hatua.

Chochote unachofanya ambacho unataka wengine wakubaliane na wewe, angalia ni nini wanachojali zaidi, kisha anza nacho katika ushawishi.
Na kwa kuwa kila mmoja wetu kuna kitu anauza, basi sehemu sahihi ya kuanzia ni kujua hitaji kubwa la wale unaowalenga na kisha kutumia hitaji hilo kuwaonesha watakavyolipata kwa kuchukua hatua au kulikosa kama hawatachukua hatua.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuwashawishi wengine kuchukua hatua kwa kuanza na manufaa yao binafsi.
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1