“I judge you unfortunate because you have never lived through misfortune. You have passed through life without an opponent—no one can ever know what you are capable of, not even you.”
—SENECA, ON PROVIDENCE, 4.3

Ni siku nyingine mpya, siku bora na ya kipekee sana kwetu.
Tumeipata nafasi hii nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.

Asubuhi ya leo tutafakari HUWEZI KUJUA UWEZO WAKO MPAKA UTAKAPOJARIBIWA.
Majaribu, magumu na changamoto unazopitia kwenye maisha ndiyo yanayokuwezesha wewe kujua uwezo mkubww uliopo ndani yako.
Kama hujawahi kukutana na magumu, huwezi kujua uwezo wako wa kupambana.

Bahati mbaya kwenye maisha siyo kukutana na magumu, bali kupita kwenye maisha bila ya magumu yoyote.
Magumu ndiyo yanakufanya uwe imara, magumu ndiyo yanakufanya ujijue wewe mwenyewe na hata uwajue wale wanaokuzunguka.
Mambo yanapokuwa mazuri, kila mtu anaweza kusema anakupenda, anakujali, yuko pamoja na wewe.
Ni pale mambo yanapokuwa magumu ndiyo unaziona rangi halisi za watu.

Hivyo lengo lako isiwe kuwa na maisha rahisi ambayo hayana magumu, bali kukabiliana na magumu ili kujijua na kuwa imara zaidi.
Kama ambavyo Nietzsche amewahi kusema, kisichokuua kinakufanya kuwa imara.
Kama ugumu unaopitia hautakuua, nasi jua utakuacha ukiwa bora kuliko ulivyokuwa hapo awali.
Hivyo usiombe kuwa na maisha rahisi, bali kuwa imara kukabiliana na kila aina ya ugumu.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kukaribisha na kukabiliana na kila aina ya ugumu, ili uwe imara na bora zaidi.
#UgumuUnakuimarisha #UsikimbilieRahisi #UtawajuaWatuWakatiWaMagumu

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1