Rafiki yangu mpendwa,

Moja ya kusudi kubwa la kuanzisha KISIMA CHA MAARIFA ni kutengeneza hadithi ya tofauti ya mafanikio kwa Watanzania na dunia kwa ujumla.

Tumezoea kujifunza kupitia vitabu vya nchi nyingine jinsi ambavyo watu wamefanikiwa, lakini kwenye mazingira yetu hadithi za aina hii ni ngumu sana kuzipata.

Hadithi zilizopo ni za ubaya tu kuhusu waliofanikiwa. Utasikia mambo mabaya tu kuhusu wale waliofanikiwa, na mengi huwa siyo ya kweli, lakini watu hao kwa sababu wapo bize na mafanikio yao, huwa nawana muda au nguvu ya kupinga habari mbaya zinazosambazwa kuhusu wao.

9D1A5635

Sasa KISIMA CHA MAARIFA kinabadili hilo kabisa, kinatengeneza hadithi mpya kabisa ya mafanikio, hadithi za ukweli za watu ambao wametoka chini na kwenye ugumu na kuweza kupiga hatua sana, kupitia kujifunza maarifa sahihi na kufanyia kazi yale ambayo wamejifunza.

Kila mwaka kwenye KISIMA CHA MAARIFA tumekuwa na semina yetu ya kukutana ana kwa ana. Semina hii imekuwa inafanyika karibu na mwisho wa mwaka wa kalenda, ambao kwetu wanamafanikio ni mwanzo wa mwaka wa mafanikio.

Mwaka huu 2019, semina hii kubwa sana itafanyika jumapili ya tarehe 03/11/2019 jijini Dar es salaam.

Semina ya mwaka huu 2019 itakuwa tofauti sana na semina za miaka iliyopita, kwani mwaka huu kutakuwa na wanenaji wengi kuliko miaka mingi. Na sehemu kubwa ya wanenaji hawa watakuwa wanamafanikio ambao wanashirikisha uzoefu wao na ushuhuda wao kwenye kile wanachofanya na kule walikotoka na kuweza kupiga hatua zaidi.

Utaondoka kwenye semina hii, ukiwa na hadithi nyingi na nzuri ambazo zinakupa mafunzo na hamasa ya kupiga hatua zaidi, ili mwaka unaofuata na wewe uwe mmoja wa wale watakaoshuhudia jinsi mwaka ulivyokwenda kwako.

UNA NAFASI YA WEWE KUSHIRIKISHA.

Rafiki, nakupa nafasi ya wewe kushirikisha uzoefu wako na ushuhuda wako wa hatua ambazo umekuwa unachukua na matokeo unayopata. Haijalishi ni makubwa au madogo kiasi gani, kama kuna matokeo ya tofauti unayapata, hiyo ni hadithi nzuri kwa wengine, maana kuna ambao wamekwama na wakisikia hadithi yako, watanufaika sana.

Hivyo basi rafiki yangu, kama una kitu ambacho unajua kinaweza kuwanufaisha wengine, nijulishe ili uweze kupata nafasi ya kukishirikisha. Kama kuna uzoefu ulionao ambao wengine wanaweza kunufaika nao tunapenda sana kuusikia. Na kama una ushuhuda wa hatua ulizopiga, karibu sana utushirikishe.

Pia kama wewe ni mwalimu, mshauri au mhamasishaji na upo kwenye KISIMA CHA MAARIFA basi karibu sana utushirikishe masomo mbalimbali unayotoa. Utaweza kupata nafasi kwenye semina ya mwaka 2019 ya kufundisha kile ulichonacho.

Pia kama una bidhaa au huduma ambazo unajua zinaweza kuwasaidia wanamafanikio, iwe ni vitabu, video, sauti na huduma nyingine ambazo wengine wanaweza kunufaika nazo, nakukaribisha pia uje na bidhaa au huduma hizo kwenye semina yetu hii. Muhimu ni iwe bidhaa au huduma uliyoitengeneza wewe mwenyewe, na siyo ya mtu mwingine unaiuza.

Kupata nafasi hizi za kushirikisha uzoefu wako, ushuhuda wako na hata bidhaa au huduma zako, tuwasiliane kwa namba 0717396253, kwa kupiga simu, kutuma ujumbe wa kawaida au ujumbe wa wasap. Karibu sana upate nafasi ya kuwashirikisha wengine, kumbuka unapofundisha kile unachojua, unakijua zaidi.

KUPATA NAFASI YA KUSHIRIKI SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2019.

Ili kupata nafasi ya kushiriki semina ya kukutana ana kwa ana ya mwaka huu 2019, kwanza kabisa lazima uwe mwanachama hai wa KISIMA CHA MAARIFA, ambaye ada yake haijaisha.

Ukishakuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, unapaswa kulipa ada ya ushiriki wa semina ambayo ni tsh 100,000/= (laki moja). Ada hii itajumuisha huduma zote utakazozipata kwa siku nzima ya semina, kuanzia kifungua kinywa, chakula cha mchana, vitafunwa vya jioni, vijitabu vya kuandika na kalamu.

Kama bado hujawa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA na ungependa kushiriki semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2019, basi jiunge sasa ili uweze kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA. Kwa kujiunga utapata manufaa mengine mengi sana, ya kujifunza pamoja na kuwa kwenye klabu za mafanikio. Kujiunga, tuma ujumbe sasa kwa wasap kwenda namba 0717396253 wenye maneno KISIMA CHA MAARIFA na utatumiwa maelekezo ya kujiunga.

MWISHO WA KUPATA NAFASI YA KUSHIRIKI.

Mwisho wa kupata nafasi ya kushiriki semina hii ya KISIMA CHA MAARIFA 2019 ni tarehe 31/10/2019, hivyo unapaswa kuwa umeshalipa ada yako ya kushiriki semina hii mpaka kufikia tarehe hiyo.

Ili kuhakikisha kila mtu anashiriki semina hii natoa nafasi ya kulipa ada kidogo kidogo ili mpaka kufikia tarehe 31/10/2019 uwe umeshakamilisha malipo yako.

Unaweza kuchagua kulipa yote tsh 100,000/= kwa mara moja mapema na hapo ukajiweka uhakika wa kushiriki semina.

Unaweza kuchagua kulipa kila mwisho wa mwezi tsh 35,000/= kuanzia mwisho wa mwezi wa nane, wa tisa na wa kumi na hapo utajihakikishia kushiriki.

Unaweza kuchagua kulipa kila mwisho wa wiki, na kila wiki ukalipa tsh 10,000/= na ukawa umemaliza malipo yako ndani ya muda huo.

Lakini pia unaweza kuchagua kulipa kila siku, kwa kulipa tsh 1,500/= na ukilipa kila siku ndani ya siku zilizobaki utajihakikishia kupata nafasi ya kushiriki semina yetu ya mwaka 2019.

HATUA ZA KUCHUKUA LEO ILI USIKOSE SEMINA HII.

Rafiki, ili kuhakikisha hukosi semina hii ya KISIMA CHA MAARIFA 2019, basi chukua hatua hii sasa, andika ujumbe wa kawaida au wasap na tuma kwenye namba 0717396253, ujumbe uwe na majina yako kamili, namba yako ya simu, barua pepe yako na maelezo kwamba utashiriki semina. Pia kwenye ujumbe huo eleza kama utalipa ada kwa siku, wiki, mwezi au mara moja, na tarehe utakayofanya hivyo.

Mfano wa ujumbe ni kama hivi; mimi Makirita Amani, simu; 0717396253, email; makirita@kisimachamaarifa.co.tz Nitashiriki semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2019, ada nitalipa kila tarehe ya mwisho wa mwezi.

Chukua hatua hiyo sasa rafiki yangu ili kuweza kujihakikishia nafasi ya kushiriki kwenye semina yetu ya KISIMA CHA MAARIFA mwaka 2019, kitu ambacho kitakupa msukumo mkubwa wa kupiga hatua zaidi kwenye maisha yako.

Asante sana rafiki yangu na nina uhakika tarehe 03/11/2019 tutakuwa pamoja kwenye semina, tuma ujumbe wako sasa wa kuthibitisha kushiriki ili usikose nafasi.

MUHIMU; Ili usisumbuke, thibitisha ushiriki wako mapema kwa kutuma ujumbe wenye majina yako, mawasiliano na mpango wako wa malipo.

Rafiki, kama ungependa kuendelea kupokea makala na mafunzo mengine mazuri kwenye email yako, fungua hapa na ujaze fomu; www.bit.ly/amkaemail

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali. Kupata Huduma Za Ukocha Tembelea; www.amkamtanzania.com/kocha