“You can bind up my leg, but not even Zeus has the power to break my freedom of choice.”
—EPICTETUS, DISCOURSES, 1.1.23
Hongera sana mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana tuliyonayo leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.
Asubuhi ya leo tutafakari WANAWEZA KUKUFUNGA MIKONO, LAKINI…
Watu wanaweza kukufunga mikono yako,
Wanaweza kukufunga miguu yako,
Wanaweza kuutesa mwili wako,
Lakini…
Lakini hakuna mwenye uwezo wa kuvunja uhuru wako wa kuchagua,
Hakuna mwenye uwezo wa kukulazimisha ufikiri nini,
Hakuna mwenye uwezo wa kukulazimisha uwe na mtazamo anaotaka yeye.
Uhuru wa kuchagua, kufikiri na mtazamo, ndiyo uhuru pekee ambao hakuna mtu yeyote mwenye uwezo wa kukunyang’anya wewe.
Ni mpaka wewe mwenyewe uchague kuwaruhusu watu kuchukua uhuru huo.
Ili kuwa na maisha bora, hakikisha unalinda uhuru huu mkubwa na muhimu kwako.
Usikubali kumpanmtu yeyote nafasi ya kuingilia uhuru huo wa kipekee kwako.
Na hiyo ndiyo falsafa ya kweli,
Kulinda uhuru wako wa kufikiri, kuamua na mtazamo hata pale mambo yanapokuwa magumu.
Kuamua unafikiri na kuchukuliaje mambo hata pale mambo yanapoonekana kuwa magumu sana.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kulinda uhuru wako, siku ya kuchagua unafikiri nini, unaamua nini na unakuwa na mtazamo gani licha ya kazingira yanayokuzunguka.
#NidhamuUadilifuKujituma #AfyaUtajiriHekima #KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1