“No one is crushed by Fortune, unless they are first deceived by her . . . those who aren’t pompous in good times, don’t have their bubbles burst with change. Against either circumstance, the stable person keeps their rational soul invincible, for it’s precisely in the good times they prove their strength against adversity.”
—SENECA, ON CONSOLATION TO HELVIA, 5.4b, 5b–6

Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana tuliyoiona leo.
Ni nafasi mpya na bora sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.

Asubuhi ya leo tutafakari USIDANGANYIKE NA BAHATI…
Mambo mazuri yanapotokea kwenye maisha yetu, huwa tunaona ni juhudi zetu, tunajiona tuna ujanja na uwezo mkubwa wa kuwezesha mambo kutokea.
Mambo mabaya yanapotokea kwenye maisha yetu, huwa tunajiona tuna bahati mbaya na kujiuliza kwa nini sisi tu.

Ukweli ni kwamba, mambo huwa yanatokea, siyo kwa sababu ya uwezo wetu au kwa bahati mbaya, bali mambo huwa yanatokea.
Hivyo unapokuwa unapitia mambo mazuri, usijisahau na kuona umeshamaliza kila kitu, kuna mambo magumu yanakusubiri na si muda mrefu yatakufikia.
Ni vyema kila wakati kuwa na maandalizi ya hali yoyote, nzuri au mbaya, rahisi au ngumu.
Kwa sababu wewe siyo mpangaji wa nini kitakachotokea.

Juhudi zako binafsi zina mchango wa kugeuza kile kinachotokea kiwe na manufaa kwako,
Lakini hazina nguvu ya kuamua kipi kitokee na kipi kisitokee.
Usidanganyike na bahati, iwe nzuri au mbaya, badala yake kila wakati kuwa na maadalizi sahihi.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuwa na maandalizi sahihi kwa lolote linaloweza kutokea na kulitumia kwa manufaa yako binafsi badala ya kulalamika kwa nini limetokea au kutokutokea.
#UsidanganyikeNaBahati #KuwaImaraNyakatiZote #HangaikaNaYaliyoNdaniYaUwezoWako

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1