Unajua kwa nini biashara nyingi zinaishia kushindwa?
Ni kwa sababu waanzilishi wa biashara hizo hawana chochote cha tofauti cha kuwavutia wateja kwenda kununua kwenye biashara hizo.
Kila kinachofanyika kwenye biashara hiyo ndiyo kinachofanyika kwenye biashara nyingine pia.
Ni kama mkakati wao wa kununua ni kuwaambia wateja njooni mnunue kwangu, mteja akiuliza kwa nini tununue kwako anajibiwa kwa sababu na mimi pia nauza.
Huu ni mkakati mbovu sana wa kuendesha biashara ambao unakuhakikishia kushindwa.
Ingia kwenye biashara ukiwa na mkakati wa kukutofautisha na wafanyabiashara wengine. Ingia ukiwa na sababu ya kuwashawishi wateja kuja kununua kwako na kuacha kule wanakonunua sasa.
Lazima ujue hilo siyo zoezi rahisi, ndiyo maana unapaswa kuweka nguvu kubwa katika kuwashawishi wateja mpaka waje kununua kwako. Unapokuwa na kitu cha tofauti, hilo linawapa uhakika wateja wako.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,