Rafiki yangu mpendwa sana,
Kuiona siku hii nyingine nzuri sana ya leo ni bahati ya kipekee sana kwetu. Hii si nafasi ya wewe kuichezea, kwa sababu siyo wote waliopanga kuiona nafasi hii wameipata. Hivyo wewe una bahati, na itumie bahati hiyo vizuri.
Siku ya leo nenda kaweke mkazo kwenye vipaumbele vyako, ufanye yale mambo ambayo ni muhimu kwako na yanayokufikisha kwenye mafanikio makubwa. Pangilia vyema siku yako kabla hujaanza kufanya chochote ili uweze kuwa na siku bora sana.
Kwenye makala hii fupi ya leo nakwenda kujibu swali moja muhimu sana kuhusu kuhudhuria SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2019 ambayo ni semina ya mwaka inayowakusanya wanamafanikio wote kutoka nchi nzima na kuwa pamoja kwa siku nzima, wakijifunza, kuhamasishana na kuweka malengo makubwa ya mwaka mzima.
Kama nilivyokupa taarifa awali, semina hii itafanyika jumapili ya tarehe 03/11/2019 jijini Dar es salaam. Kama hukupata maelezo kwa kinakuhusu semina hii nitayarudia tena mwisho wa makala hii.
Wapo watu wamekuwa wakifikiri na wengine kuuliza au kufikia maamuzi kwamba, kwa sababu mtu anasoma vitabu nilivyoandika, kwa sababu mtu anasoma makala nyingi ninazoandika kila siku, basi hakuna haja ya kuhudhuria semina. Kwa sababu mambo atakayokwenda kujifunza ni yale yale anayosoma kwenye vitabu na makala.
Na hapa ndipo wengi wanakosea na kukosa fursa nzuri sana ya kujifunza na kuchukua hatua kupitia semina mbalimbali.
Kuhudhuria semina ni tofauti kabisa na kusoma vitabu au makala. Hata kama semina itakuwa imetoa mafundisho yake kwenye kitabu fulani. Bado kuhudhuria semina utaondoka na mambo wengi kuliko kusoma kitabu pekee.
Kwenye semina kuna ile hali ya uwepo wa moja kwa moja kwenye mafunzo, kujifunza na kuchukua hatua, kitu ambacho hakipatikani kwenye kusoma makala au vitabu.
Kwa mfano, watu wengi wamekuwa hawasomi kitabu mpaka mwisho. Na hata wale wanaosoma, ni wachache sana wanaofanya mazoezi au kuchukua hatua zinazokuwa zimeshauriwa kwenye kitabu husika. Wengi husoma ili tu kumaliza, au husoma huku wakiwa wanaelekea kufanya vitu vingine.
Makala ndiyo kabisa watu hawazisomi kwa kina, wengi huweza kufungua na kusema watasoma vizuri zaidi baadaye, wakajikuta wamefungua nyingi na hakuna hata moja wamesoma. Wengine huangalia zile pointi muhimu na kuendelea na mambo yao.
Lakini unapohudhuria kwenye semina, hasa semina ya siku nzima kama ya KISIMA CHA MAARIFA, unakuwa upo pale kwenye semina, huna pengine pa kukimbilia, unahitaji kukaa na kujifunza. Utasikiliza na kuchukua hatua ya yale unayojifunza kwa sababu huna unakokimbilia.
Nguvu nyingine ya semina ni uwepo wa watu wengine. Unaposoma vitabu na makala, mara nyingi unakuwa mwenyewe, hivyo unakosa ile hali ya upamoja ambayo inapatikana kwenye semina. Unapohudhuria semina, unakutana na watu wengine, ambao wana mtazamo kama wako, na hivyo kwa pamoja mnajifunza. Uwepo wa wengine unakuhamasisha, na kukuwezesha kuchukua hatua kwa pamoja.
Semina pia inaongeza na kukuza mtandao wako wa watu unaowafahamu na wanaokufahamu. Dunia ya sasa inabadilika sana, siyo tena unajua nini bali unamjua nani na nani anakujua wewe. Na siyo kwa nia mbaya kwamba ni rushwa au upendeleo, bali unapojuana na watu wengi, unapata taarifa nyingi. Na pale unaowajua na wanaokujua wanapokuwa watu waaminifu na wenye tabia nzuri, mnaweza kushirikiana kwenye shughuli nyingine kama biashara na hata kazi.
Hivyo rafiki yangu, kuhudhuria semina za moja kwa moja, ni muhimu sana hata kama unasoma vitabu na makala nyingi kila siku. Kuna ‘upako’ wa kisemina ambao unapatikana kwenye semina, kama ambavyo kusoma Biblia au Kuran hakukufanyi usiende kanisani au msikitini.
Nakumbuka kwenye semina ya mwaka 2018, kuna mtu mmoja alikuwa anatokea mbali sana, hivyo akaniambia haoni umuhimu wa kuhudhuria kwa sababu mengi ameshajifunza. Nikamwambia unafanya kosa kubwa sana kutokuhudhuria, nilimwambia ahudhurie tu, halafu mwisho aniambie kama ameona tofauti. Baada ya semina kuisha alinifuata akaniambia Kocha nashauri hizi semina ziwe zinafanyika mara mbili kwa mwaka, kwa sababu nimepata nguvu kubwa sana kwenye semina hii.
Rafiki, kama na wewe unataka kupata ‘upako’ huu wa kimafanikio unaopatikana kwa kushiriki semina, basi usikose SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2019. Kwa sababu hii ni semina ambayo itawasha moto mkali wa mafanikio ndani yako, ambao utaweza kukusukuma kwa mwaka mzima unaofuata.
Maelezo kuhusu semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2019 yako hapo chini.
KARIBU KWENYE SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2019.
Rafiki yangu mpendwa, tutakuwa na semina ya KISIMA CHA MAARIFA ya mwaka 2019 ambayo itafanyika siku ya jumapili ya tarehe 03/11/2019. Semina ya mwaka huu 2019 itafanyika jijini dar es salaam, eneo kamili itajulishwa baadaye. Itakuwa ni semina ya siku nzima, itakayoanza saa moja kamili asubuhi mpaka saa moja kamili usiku.
Kwenye semina hii tutapata mafunzo ya kina kutoka kwa kocha Dr Makirita Amani, pia tutapata kujifunza kutoka kwa walimu wengine. Na sehemu muhimu zaidi ya semina hii ni kwamba tutapata nafasi ya kujifunza kutoka kwa wanamafanikio wenzetu, kupata shuhuda halisi za jinsi ambavyo wenzetu wanapiga hatua kwenye maisha yao.
Semina hii inawakusanya wanamafanikio wote kutoka kila kona ya Tanzania na wengine kutoka nchi jirani, ambao wanakuja pamoja na kujifunza kwa kina kwa siku moja na kuondoka na nguvu na hamasa kubwa ya kuchukua hatua ili kufanikiwa zaidi.
Kwenye semina ya mwaka huu 2019 tutakwenda kupata shuhuda nyingi sana kutoka kwa wenzetu ambao wamepiga hatua mbalimbali, kuanzia walipotoka na jinsi ambavyo wameweza kupiga hatua kupitia maarifa wanayopata pamoja na huduma nyingine wanazopata kama huduma za ukocha.
KUPATA NAFASI YA KUSHIRIKI SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2019.
Ili kupata nafasi ya kushiriki semina ya kukutana ana kwa ana ya mwaka huu 2019, kwanza kabisa lazima uwe mwanachama hai wa KISIMA CHA MAARIFA, ambaye ada yake haijaisha.
Ukishakuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, unapaswa kulipa ada ya ushiriki wa semina ambayo ni tsh 100,000/= (laki moja). Ada hii itajumuisha huduma zote utakazozipata kwa siku nzima ya semina, kuanzia kifungua kinywa, chakula cha mchana, vitafunwa vya jioni, vijitabu vya kuandika na kalamu.
Kama bado hujawa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA na ungependa kushiriki semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2019, basi jiunge sasa ili uweze kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA. Kwa kujiunga utapata manufaa mengine mengi sana, ya kujifunza pamoja na kuwa kwenye klabu za mafanikio. Kujiunga, tuma ujumbe sasa kwa wasap kwenda namba 0717396253 wenye maneno KISIMA CHA MAARIFA na utatumiwa maelekezo ya kujiunga.
MWISHO WA KUPATA NAFASI YA KUSHIRIKI.
Mwisho wa kupata nafasi ya kushiriki semina hii ya KISIMA CHA MAARIFA 2019 ni tarehe 31/10/2019, hivyo unapaswa kuwa umeshalipa ada yako ya kushiriki semina hii mpaka kufikia tarehe hiyo.
Ili kuhakikisha kila mtu anashiriki semina hii natoa nafasi ya kulipa ada kidogo kidogo ili mpaka kufikia tarehe 31/10/2019 uwe umeshakamilisha malipo yako.
Unaweza kuchagua kulipa yote tsh 100,000/= kwa mara moja mapema na hapo ukajiweka uhakika wa kushiriki semina.
Unaweza kuchagua kulipa kila mwisho wa mwezi tsh 35,000/= kuanzia mwisho wa mwezi wa nane, wa tisa na wa kumi na hapo utajihakikishia kushiriki.
Unaweza kuchagua kulipa kila mwisho wa wiki, na kila wiki ukalipa tsh 10,000/= na ukawa umemaliza malipo yako ndani ya muda huo.
Lakini pia unaweza kuchagua kulipa kila siku, kwa kulipa tsh 1,500/= na ukilipa kila siku ndani ya siku zilizobaki utajihakikishia kupata nafasi ya kushiriki semina yetu ya mwaka 2019.
HATUA ZA KUCHUKUA LEO ILI USIKOSE SEMINA HII.
Rafiki, ili kuhakikisha hukosi semina hii ya KISIMA CHA MAARIFA 2019, basi chukua hatua hii sasa, andika ujumbe wa kawaida au wasap na tuma kwenye namba 0717396253, ujumbe uwe na majina yako kamili, namba yako ya simu, barua pepe yako na maelezo kwamba utashiriki semina. Pia kwenye ujumbe huo eleza kama utalipa ada kwa siku, wiki, mwezi au mara moja, na tarehe utakayofanya hivyo.
Mfano wa ujumbe ni kama hivi; mimi Makirita Amani, simu; 0717396253, email; makirita@kisimachamaarifa.co.tz Nitashiriki semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2019, ada nitalipa kila tarehe ya mwisho wa mwezi.
Chukua hatua hiyo sasa rafiki yangu ili kuweza kujihakikishia nafasi ya kushiriki kwenye semina yetu ya KISIMA CHA MAARIFA mwaka 2019, kitu ambacho kitakupa msukumo mkubwa wa kupiga hatua zaidi kwenye maisha yako.
Asante sana rafiki yangu na nina uhakika tarehe 03/11/2019 tutakuwa pamoja kwenye semina, tuma ujumbe wako sasa wa kuthibitisha kushiriki ili usikose nafasi.
MUHIMU; Ili usisumbuke, thibitisha ushiriki wako mapema kwa kutuma ujumbe wenye majina yako, mawasiliano na mpango wako wa malipo.
Rafiki na kocha wako,
Dr. Makirita Amani.