“Difficulties show a person’s character. So when a challenge confronts you, remember that God is matching you with a younger sparring partner, as would a physical trainer. Why? Becoming an Olympian takes sweat! I think no one has a better challenge than yours, if only you would use it like an athlete would that younger sparring partner.”
—EPICTETUS, DISCOURSES, 1.24.1–2
Ni siku nyingine nzuri tumeiona leo, nafasi ya kipekee kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.
Asubuhi ya leo tutafakari HAKUNA FAIDA BILA YA MAUMIVU…
Leo tutafakari kupitia maswali, maswali ya kujidadisi na kupata hasa mzizi wa matokeo tunayopata sasa.
Hivi unakuwa unafikiria nini pale unapojiambia unataka kupata mafanikio nakubwa, lakini pia unataka uwe na maisha ya kawaida kama watu wengine?
Kwamba ufanye kazi/biashara kama wanavyofanya wengine, kwa muda sawa na wao, uwe na mapumziko kama wao, ununue vitu wanavyonunua wao halafu mwisho wa siku uwe umepiga hatua kuliko wao!
Huwa unafikiriaje pale unapokuwa unaweka mipango yako, halafu kutegemea kila kitu kiende kama unavyotaka? Kwamba siku hizi dunia inakusikiliza wewe na kuenda kwa matakwa yako?
Inakuwaje mpaka mawazo ya mafanikio makubwa bila ya kujichosha, kama wale wanaokuwa wanauliza ni biashara gani ya uhakika, yenye faida kubwa kwa haraka na isiyochosha wanaweza kufanya. Hivi unafikiri biashara ya aina hiyo ingekuwepo mpaka sasa ingekuwa inakusubiri jiniazi wewe uje uivumbue?
Rafiki, ninachotaka uelewe hapa ni kwamba, matokeo unayopata sasa, iwe ni kifedha au hatua ulizopiga, ni sawasawa na maumivu uliyopitia huko nyuma.
Kama umekuwa unakwepa maumivu basi matokeo yako yatakuwa ni madogo.
Kama umekuwa hupendi kuwa tofauti na wenyine, hutaki kuonekana una maisha ya ajabu, basi umeweka nguvu kuzalisha maisha ya kwaida na yanayokutesa sasa.
Kama unataka kufika mbali zaidi ya hapo ulipo sasa, maumivu lazima yahusike, lazima upitie maisha ambayo wengine wanakuambia ni ya ajabu na yasiyofaa.
Kwa kifupi, kama kila unachofanya wengine nao wanaweza kufanya na wanakubaliana na wewe, basi unafanya makosa, ni kitu ambacho hakiwezi kukufikisha kwenye mafanikio makubwa.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kufanya yale magumu na yenye maumivu, kwa sababu hayo ndiyo yenye manufaa makubwa kwako na kukuwezesha kufanikiwa zaidi.
#MatokeoUnayopataNiGharamaUliyolipa #KuwaKawaidaNiKushindwa #KataaKufuataKundi
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1
Asante sana kocha uko sahihi sana. Matokeo yetu yanafanana na gharama ambazo tumeamua kulipa..
LikeLike
Ndiyo.
LikeLike