“Meditate often on the interconnectedness and mutual interdependence of all things in the universe. For in a sense, all things are mutually woven together and therefore have an affinity for each other—for one thing follows after another according to their tension of movement, their sympathetic stirrings, and the unity of all substance.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 6.38

Kupata nafasi nyingine nzuri kama hii ya leo ni jambo la kushukuru sana.
Hatujaiona siku hii kwa akili na nguvu zetu, bali ni bahati.
Hivyo tunapaswa kuitumia siku hii vizuri, tufanyie kazi vipaumbele vyetu na kuachana na yasiyo muhimu.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.

Asubuhi ya leo tutafakari TUNATEGEMEANA…
Vitu vyote hapa duniani vinategemeana ili kuweza kuikamilisha dunia na maisha kwa ujumla.
Hakuna awezaye kusema kwamba amejitosheleza yeye mwenyewe.
Hakuna anayeweza kufanya kila kitu peke yake bila ya kuwategemea wengine na vitu vingine.
Hakuna jeshi la mtu mmoja.
Ili ufanikiwe, unahitaji ushirikiano mzuri wa watu wengi na vitu mbalimbali.
Hivyo una wajibu mkubwa wa kutengeneza mahusiano bora na kila unayehusika naye.
Pia kutumia vizuri kila kinachokuzunguka, kwa sababu vyote vina mchango kwenye mafanikio yako.

Usimdharau mtu yeyote wala kitu chochote,
Unaweza kuona hana umuhimu kwa sasa, lakini kuna wakati utamhitaji sana katika kukamilisha mambo muhimu.
Wekeza katika kujenga na kuimarisha mahusiano yako na wengine.
Na pia kazana kutumia vizuri kila kinachokuzunguka ili kuweza kupiga hatua zaidi.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kutengeneza mahusiano bora na wengine na kutumia vizuri kila kinachokuzunguka ili uweze kufanikiwa zaidi.
#UnachotakaKipoKwaWengine #HaijalishiUnajuaNiniBaliUnamjuaNani #ImarishaMahusianoYako

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1