Rafiki yangu mpendwa,
Zipo siri nyingi sana za mafanikio, na japo zinaitwa siri, huwa ni vitu vya wazi, kabisa. Ila kwa kuwa wengi hawapo tayari kuchukua hatua wanazopaswa kuchukua ili kufanikiwa basi hatua hizo zinaonekana ni siri.
Siri za mafanikio zilizozoeleka ni kufanya kazi kwa juhudi, kuwa mbunifu na kufanya kwa utofauti, kuwa mvumilivu na king’ang’anizi, kutokukata tamaa na kujifunza kutoka kwa waliofanikiwa. Siri hizi huwa zinahubiriwa na kila mtu, na zipo wazi, japo siyo kila mtu anayeweza kuzifanyia kazi.
Kuna siri moja ya mafanikio ambayo ni muhimu sana, lakini hakuna anayechukua muda wake kukusisitizia kama ilivyo kwa siri nyingine za mafanikio. Ukiielewa siri hii moja na kuifanyia kazi, utaweza kuwa mbali sana na wengine inapokuja kwenye swala la mafanikio.
Kabla sijakuambia siri hiyo muhimu na hatua za kuchukua ili kuifaidi siri hiyo, hebu kwanza nikuoe mfano wa hatua ambazo umekuwa unachukua.
Hebu niambie, ni wakati gani ambapo huwa unaweka malengo na mipango yako ya mwaka?
Najua jibu lipo wazi, wakati wa mwaka mpya, ndiyo huwa unafanya hivyo. Wakati huo kila mtu anakuwa anazungumzia malengo na mipango mikubwa, hivyo na wewe unabebwa na mkumbo huo, na kujikuta unaweka malengo na mipango ambayo siyo yako. Malengo na mipango unayojiwekea wakati wa mwaka mpya inakuwa siyo yako kwa sababu unaingiliwa na ushawishi wa wengine ambao nao wanafanya hivyo.
Ndiyo maana mwezi mmoja baada ya mwaka kuanza, asilimia 90 ya watu wanaokuwa wamejiwekea malengo na mipango ya mwaka huo, wanakuwa wameshaachana nayo na kurudi kwenye maisha ya kawaida.
Sasa siri kubwa ya mafanikio ninayokwenda kukushirikisha hapa leo, inakwenda kuondoa kabisa hali hiyo ya kuweka malengo na mipango kwa kufuata mkumbo, na kuweza kufanya jambo hilo muhimu ukiwa na utulivu wa ndani.
Rafiki yangu mpendwa, sasa umefika wakati wa mimi kukupa siri pekee ya mafanikio ambayo hakuna anayekusisitizia sana. Siri hiyo ni hii; kwa chochote unachofanya, kuwa mbele ya wengine.
Hiyo ndiyo siri, kuhakikisha kila unachofanya basi uko mbele ya wengine. Kwenye kazi, biashara, maisha, kila kitu, kuwa mbele kabisa ya wengine. Usikubali kufuata mkumbo au kuwa katikati ya kundi kubwa la watu, wewe kuwa mbele kabisa, na waache wengine wote nyuma.
Unapokuwa mbele ya wengine, unaona vizuri kule unakokwenda kuliko ukiwa katikati ya kundi kubwa la watu. Pia juhudi unazoweka haziingiliwi na usumbufu wa wengine. Mipango unayoweka inakuwa yako kweli na juhudi unazochukua zinaendana na mipango hiyo.
Jinsi ya kuitumia siri hii kufanikiwa zaidi.
Rafiki, kila mwaka nimekuwa nakushauri kuweka malengo na mipango yako mapema kabla ya wengine hawajaanza kufanya hivyo. Hii ndiyo siri ya kuwa mbele ya wengine.
Kwa kuwa kila mtu huwa anaweka malengo na mipango yake ya mwaka mzima mwezi januari, ambapo kila mtu anakuwa anafanya hivyo, mimi nimekuwa nakushauri wewe kuwahi kufanya zoezi hilo. Na muda sahihi kwako kufanya zoezi hilo ni mwezi novemba.
Yaani malengo na mipango yako ya mwaka 2020 hupasi kuiweka januari 2020, badala yake unapaswa kuyaweka mwezi novemba 2019. Hii inakusaidia kuwa na utulivu wakati wa kuweka malengo yako na kutokusumbuliwa na msukumo wa nje. Lakini pia inakupa muda mzuri wa kukutosha wewe kuanza kufanyia kazi malengo yako kabla ya wengine.
Na kizuri zaidi kwenye mfumo huu ni kwamba, mwisho wa mwaka watu wengi huwa wanapunguza sana juhudi wanazoweka, na hivyo kama wewe ndiyo umeweka malengo yako, na kuanza kuyafanyia kazi mwisho wa mwaka, unakuwa na uwanja mpana wa kufanya vizuri kwa sababu wengine wote wanakuwa wamechoka na kupunguza kasi.
KARIBU TUUANZE PAMOJA MWAKA MPYA 2020.
Kupitia dhana hii ya kuuanza mwaka mpya mapema, tumekuwa na semina za mwaka kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Inapofanyika semina hii ndiyo wakati sahihi kwetu kuuanza mwaka mpya wa mafanikio.
Na katika kuuanza mwaka mpya wa 2020 kwa mafanikio zaidi, tarehe 03/11/2019 tutakuwa na semina yetu ya KISIMA CHA MAARIFA 2019, ambapo tunakwenda kuuanza pamoja mwaka wa mafanikio 2019/2020.
Wakati wengine wameshapumzika na kujiambia wataanza vizuri mwaka 2020 utakapoanza, sisi tunakwenda kuuanza mwaka huo kwa moto mkubwa, miezi miwili kabla wengine hawajastuka kutoka kwenye usingizi waliolala.
Karibu sana kwenye semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2019, ambapo pamoja na kupata nafasi ya kuuanza mwaka wa mafanikio mapema, utakwenda kujifunza na kuhamasika kupitia masomo mbalimbali yatakayokuwepo kwenye semina hii pamoja na shuhuda za wengine ambao wanachukua hatua mbalimbali.
Kama nilivyokushirikisha hapo juu, semina itafanyika siku ya jumapili, tarehe 03/11/2019, jijini Dar es salaam.
Ada ya kushiriki semina hii ni tsh laki moja (100,000/=) na unapaswa kuilipa kabla ya tarehe 31/10/2019.
Ili kuhakikisha hukosi semina hii muhimu sana kwako kwenda kuanza mwaka wa mafanikio wakati wengine bado wamelala, unapaswa kutuma ujumbe wenye majina yao na kwamba utashiriki semina hii. Ujumbe utume kwenda namba 0717396253.
Karibu sana rafiki yangu tuuanze mwaka mpya 2020 mapema wakati wengine bado hawajafikiria kufanya hivyo, na hilo linatuwezesha sisi kuwa mbele ya wengine na hivyo kutokusumbuliwa na fujo zao. Tuma sasa ujumbe wa kujiwekea nafasi ya kushiriki semina hii, ujumbe uende kwenye namba 0717396253.
Rafiki, kama ungependa kuendelea kupokea makala na mafunzo mengine mazuri kwenye email yako, fungua hapa na ujaze fomu; www.bit.ly/amkaemail
Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali. Kupata Huduma Za Ukocha Tembelea; www.amkamtanzania.com/kocha