“That which isn’t good for the hive, isn’t good for the bee.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 6.54
Ni siku nyingine nzuri, siku mpya na ya kipekee sana kwetu.
Tumeipata nafasi bora kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.
Asubuhi ya leo tutafakari MMOJA KWA AJILI YA WOTE NA WOTE KWA AJILI YA MMOJA…
Viumbe wote hapa duniani tunategemeana sana kwa ajili ya maisha kuweza kwenda.
Binadamu wote tunategemeana kwa mafanikio ya kila mmoja wetu.
Kitu chochote unachofanya chenye madhara kwa wengine, jua kina madhara kwako pia.
Unapowaibia wengine, jua unajiibia wewe mwenyewe.
Unapowaumiza wengine, jua unajiumiza wewe mwenyewe.
Kwa sababu maisha yote hapa duniani ni kitu kimoja, tutafanikiwa zaidi tukiwa na ushirikiano kuliko ushindani.
Watendee wengine vile ambavyo ungependa wakutendee wewe na kila wakati utakuwa kwenye nafasi nzuri ya kupiga hatua zaidi wewe na wale wanaokuzunguka. Kwa sababu sisi tupo kwa ajili ya wengine na wengine wapo kwa ajili yetu. Ushirikiano ndiyo utakaotuwezesha kuvuka.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuwajali wengine kama unavyojijali wewe mwenyewe, kuwatendea wengine kile ambacho ungependa wakutendee na kutengeneza ushirikiano mzuri na wengine.
#MaishaNiMfumoMmoja #UshirikianoNiMuhimu #UsiwafanyieWengineUsichopendaKufanyiwa
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1