Kinachowatofautisha matajiri na masikini kwenye fedha siyo kipato wanachoingiza, bali ni mtazamo walionao kwenye kipato wanachoingiza.
Masikini wana mtazamo wa kufanyia kazi fedha, na ndiyo maana wanachofikiria wao ni kuajiriwa na kufanya kazi muda wao wote na kulipwa kulingana na kazi waliyofanya. Mtazamo huu unawaingizia kipato kizuri, lakini kinakuwa na ukomo. Kwa sababu una masaa 24 tu kwenye siku yako na una miaka michache ya kuweza kufanya kazi kwa juhudi, mwili unachoka na huwezi kujituma tena.
Matajiri wana mtazamo wa kuifanya fedha iwafanyie wao kazi, ndiyo maana wao hufikiria biashara na uwekezaji zaidi. Wanatengeneza mfumo ambao unaweza kuzalisha fedha bila ya wao kuwepo moja kwa moja. Mwanzoni mambo huwa ni magumu kwao, kwa sababu kipato kinakuwa siyo cha uhakika kama kwa wale walioajiriwa, lakini mfumo wanaoujenga unapokamilika, wananufaika sasa.
Ukichukua watu wawili, ambao wana umri sawa, mmoja kaanzisha biashara na kuijenga vizuri na mwingine kaajiriwa, wote wakajituma kwa miaka 20, ukija kuwaangalia, wa biashara atakuwa anazidi kukuza kipato chake huku wa ajira atakuwa anazidi kuzama kwenye madeni.
Huo ndiyo uhalisia, japo umekuwa hauoneshwi wazi, kwa sababu watu hawataki ujue ukweli, ili waendelee kukutumia ipaswavyo.
Sasa mimi rafiki yako, nimejipa wajibu wa kuhakikisha wewe unapata maarifa sahihi ili uweze kufanya maamuzi sahihi ya maisha yako. Na moja ya maarifa ambayo wewe unayahitaji sana ni upande wa FEDHA.
Watu wengi hawana maarifa sahihi ya kifedha, wengi wanaishi kifedha kwa mazoea, kama ambavyo wazazi wao walikuwa wanaishi, na ndiyo maana utakuta waliotokea kwenye umasikini wanaendelea kubaki kwenye umasikini.
Kukusaidia wewe uondoke kwenye mtego huo, Nimeandika kitabu kizuri sana kwako, kinaitwa ELIMU YA MSINGI YA FEDHA.
Kitabu hiki kina maarifa yote ya kifedha, kuanzia kuongeza kipato, kudhibiti matumizi, kuweka akiba, kuwekeza, kuondoka kwenye madeni, kuwa na biashara, kulinda utajiri wako, kuwafundisha watoto elimu ya kifedha, kuandaa wosia na kutoa kwa wenye uhitaji.
Ni kitabu ambacho kitakupa msingi wa kufanya maamuzi sahihi kifedha, ambayo yatakusaidia sana kuweza kupiga hatua kwenye maisha yako.
Kama bado hujasoma kitabu hiki cha ELIMU YA MSINGI YA FEDHA, hebu chukua hatua leo rafiki yangu. Kitabu kinapatikana kwa nakala ngumu (HARD COPY) na utaweza kuletewa au kutumiwa popote pale ulipo nchini Tanzania.
Kupata kitabu, piga simu 0678 977 007 leo hii na upate kitabu na utakuwa umepiga hatua ya kwanza kuondoka kwenye umasikini.
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa.
Kocha Dr. Makirita Amani,