“When the standards have been set, things are tested and weighed. And the work of philosophy is just this, to examine and uphold the standards, but the work of a truly good person is in using those standards when they know them.”
—EPICTETUS, DISCOURSES, 2.11.23–25

Kupata nafasi ya kuiona siku hii nyingine mpya ya leo ni jambo la kushukuru sana.
Siyo wote wameweza kuiona siku hii, hivyo tunapaswa kuitumia vizuri, kwa kufanyia kazi vipaumbele vyetu.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.

Asubuhi ya leo tutafakari JIWEKEE VIWANGO NA VIISHI KILA SIKU…
Kama unataka kuwa na maisha bora na yenye msimamo,
Basi unapaswa kujiwekea viwango kwenye maisha yako na kuviishi kila siku.
Viwango hivyo ndiyo vinakuongoza ni nini unafanya na nini hufanyi.
Unapokuwa na viwango huyumbishwi na kila ambacho wengine wanafanua, bali unakuwa na msimamo wa kipi sahihi kwako kufanya.

Ukikosa viwango unakosa msimamo, unajikuta unasikiliza maoni na ushauri wa kila mtu na utalazimika kufanya kitu ambacho wewe mwenyewe unajua siyo sahihi, lakini kwa kuwa kila mtu anafanya, basi unaona siyo vibaya na wewe kufanya.
Lakini kumbuka, kama kitu siyo sahihi, kufanywa na wengi hakukigeuzi kuwa sahihi.

Jiwekee viwango kwenye kila eneo la maisha yako,
Kwenye kazi yako weka viwango vya ubora wa kazi utakayokuwa unazalisha na usishuke chini ya hapo, hata iweje.
Kwenye biashara yako weka viwango vya thamani ma huduma ambayo mteja wako atakuwa anapata na usikubali kushuka chini ya viwango hivyo.
Na kwenye maisha yako kwa ujumla jiwekee viwango vya nidhamu, mahusiano, muda, fedha na mengine, ili uweze kujisukuma kusimamia viwango hivyo kila mara.

Bila viwango, unakuwa kama bendera ambayo haina msimamo bali inafuata upepo. Usipokuwa na msimamo, hakuna anayeweza kukuamininna kukutegemea.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kujiwekea viwango kwenye kila eneo la maisha yako na kuviishi viwango hivyo kila siku.
#MaishaYaViwango #JisukumeZaidi #UsifuateMkumbo

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1