“Since habit is such a powerful influence, and we’re used to pursuing our impulses to gain and avoid outside our own choice, we should set a contrary habit against that, and where appearances are really slippery, use the counterforce of our training.”
—EPICTETUS, DISCOURSES, 3.12.6

Ni jambo la kushukuru sana kwa sisi kupata nafasi hii ya kuiona siku hii mpya ya leo.
Ni kwa bahati tu tumeiona siku hii, siyo kwa akili zetu wala ujanja wetu.
Hivyo tunapaswa kuitumia siku hii vizuri, tusiipoteze kwa mambo yasiyo na umuhimu kwetu.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.

Asubuhi ya leo tutafakari TABIA NZURI ZINAONDOA TABIA MBAYA…
Kama kuna tabia fulani ambayo unayo, na hupendezwi na tabia hiyo hivyo unataka kuibadili, ukipanga kupambana na tabia hiyo utashindwa.
Ukijiambia unaiacha tabia hiyo ndiyo itazidi kuota mizizi na kuwa sugu kwako.
Njia bora ya kuondokana na tabia usiyoipenda ni kutengeneza tabia inayopingana nayo.
Kama una tabia mbaya unayotaka kuondokana nayo, tengeneza tabia nzuri itakayochukua nafasi ya tabia hiyo mbaya.
Kwa kufanya hivyo itakuwa rahisi kubadili tabia hiyo.

Kubadili tabia kwa kukazana kuacha tabia usiyoipenda huwa hakufanyi kazi kwa sabahu unatengenezwa ombwe ambalo lisipozibwa tabia unayoiacha inarudi tena.
Lakini unapobadili tabia kwa kujijengea tabia mpya inayokinzana na ile unayotaka kuibadili hakuna ombwe unalotengeneza, na hivyo inakuwa rahisi kwako.

Kwa muda na nafasi ile ile uliyokuwa unafanya tabia usiyoipenda, weka tabia mpya.
Kama umekuwa na tabia ya ulevi na unataka kuiacha, kwa muda na nafasi hiyo hiyo ambayo umekuwa unatumia kulewa, weka tabia nyinyine mpya ambayo itakuweka bize.
Kadhalika kwenye tabia nyingine unazotaka kuondokana nazo, weka tabia mpya inayokuweka bize kwenye ule muda na nafasi uliyokuwa unatumia kufanua tabia unayotaka kuondokana nayo.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuachana na tabia usizozipenda kwa kutengeneza tabia mpya za kuchukua nafasi za tabia hizo.
#JijengeeTabiaBora #UsipiganeNaTabiaTafutaMbadala #UnawezaKubadiliTabiaYoyote

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1