Nenda shule, soma kwa bidii, faulu vizuri na utapata kazi nzuri, yenye maslahi mazuri na utakayoifanya mpaka kustaafu kwako, na baada ya hapo utapata mafao mazuri ya kukuwezesha kuishi maisha yako ya uzeeni vizuri.

Huu ni ushauri ambao umekuwa unatolewa kwa nia njema sana, na wengi wamekuwa wanaufuata, lakini matokeo yanayopatikana yamekuwa tofauti kabisa na ushauri unavyoeleza. Ushauri huu ulifanya kazi vizuri sana miaka 50 iliyopita, lakini kwa sasa, haufanyi tena kazi.

Wote tunaona jinsi ambavyo waliosoma ni wengi kuliko nafasi za ajira zinazopatikana, hivyo hata usome kwa juhudi na kufaulu vizuri, huna uhakika wa kupata kazi.

Kwa wale wachache ambao wanapata kazi, kipato cha mshahara kimekuwa hakitoshelezi mahitaji yao, gharama za maisha zimekuwa zinapanda kila siku huku kipato kikiwa hakiongezeki kwa kasi. Hili limepelekea maisha ya waajiriwa wengi kuwa magumu. Yamekuwa ni maisha ya kukopa na kulipa pale wanapopata mshahara, halafu wanaanza kukopa tena mpaka mshahara mwingine unapotoka walipe.

Wote tunaona jinsi ambavyo ajira kwenye sekta zote, za umma na binafsi zimekuwa ngumu. Kipindi cha nyuma watu waliamini kwamba ukishapata ajira kwenye sekta ya umma basi umeshayashinda maisha. Kwa sababu ilikuwa ni ajira ya uhakika mpaka kufa, kila mwaka kulikuwa na ongezeko la mshahara na kulikuwa na marupurupu mengi.

Lakini iko wazi sasa, ajira mpaka kwenye sekta za umma zimekuwa changamoto, watu wanafukuzwa kazi, hakuna ongezeko la mshahara na hakuna marupurupu zaidi ya mshahara ambao hautoshelezi mahitaji.

Kwa hali ilivyo, unaweza kulalamika kadiri utakavyo na hakuna anayeweza kukulaumu. Lakini utakachogundua ni kwamba, malalamiko yako hayatabadili ugumu wa maisha yako. Bado mshahara wako utaendelea kuwa mdogo na bado gharama za maisha zitaendelea kuwa juu.

makirita cover 3-01.jpg

Hivyo mimi rafiki yako, nimekuja na njia ya tofauti kwako, njia ya kukusaidia kuondoka kwenye mkwamo wa kipato ulionao sasa unaotokana na mshahara kuwa mdogo huku mahitaji kuwa makubwa.

Njia ambayo nakushauri uifanye ni kuwa na BIASHARA NDANI YA AJIRA. Yaani uanzishe biashara yako ya pembeni huku ukiendelea na ajira yako, uweze kuikuza na iwe sehemu ya wewe kuingiza kipato cha ziada.

Hii ndiyo njia pekee inayoweza kukupa uhuru wa maisha yako, na hata baadaye kukupa nguvu ya kuondoka kwenye ajira yako.

Lakini wote tunajua jinsi ilivyo vigumu kuanzisha biashara ukiwa umeajiriwa. Kwanza kuna swali la biashara gani unayoweza kufanya, halafu linakuja swali unapata wapi mtaji wakati kipato cha sasa hakikutoshi? Maswali mengine ya msingi ni kuhusu muda, unapataje muda wa kuendesha biashara huku bado mwajiri anachukua muda wako mwingi?

Maswali yote haya yana majibu sahihi ambao unaweza kuyafanyia kazi na ukaweza kuanzisha na kukuza biashara yako huku ukiendelea na ajira uliyonayo sasa.

Kwenye toleo la pili la kitabu cha BIASHARA NDANI YA AJIRA, nimekushirikisha maarifa sahihi unayoweza kuyatumia kuanzisha na kukuza  biashara yako ukiwa kwenye ajira.

Kitabu hiki kina sura kumi, ambazo zote zimejaa maarifa unayohitaji ili kutoka hapo ulipokwama sasa.

Sura ya kwanza inakuonesha kwa nini umefika hapo ulipo sasa na kwa nini ajira ni sehemu nzuri kwako kuanza biashara.

Sura ya pili inakupa faida kumi za kuanza biashara ukiwa kwenye ajira, hapa utaona kwa nini kama upo kwenye ajira, unapaswa kuwa na biashara ya pembeni.

Sura ya tatu inakufundisha jinsi ya kupata wazo bora la biashara kwako, wazo ambalo linaendana na wewe na ambalo utaweza kufanya makubwa.

Sura ya nne utajifunza jinsi unavyoweza kupata mtaji wa kuanza biashara ukiwa kwenye ajira. Pia itajifunza jinsi unavyoweza kuanza biashara bila ya mtaji kabisa.

Sura ya tano utajifunza jinsi ya kupata muda wa kutosha kuendesha biashara na ajira kwa wakati mmoja, hapa utaona jinsi masaa yako 24 ya siku yanatosha kufanya mambo makubwa.

Sura ya sita utajifunza jinsi ya kutengeneza mfumo wa kuiendesha biashara yako ambao utakupa wewe uhuru, kwa kuwa na mfumo, hutahitaji kufanya kila kitu kwenye biashara yako, na pia hutahitaji kuwepo muda wote.

Sura ya saba utapata michanganuo ya biashara 12 unazoweza kuanza kufanya. Biashara hizi zinaanzia ambazo hazihitaji mtaji kabisa, kisha za mitaji midogo kama elfu 50, laki 1 mpaka milioni 1. Kisha kuna za mitaji mikubwa kuanzia milioni 10 mpaka 20. Michanganuo yote hii ni kutoka kwa watu ambao wanafanya biashara hizo, hivyo unajifunza kutoka kwa wafanyaji kabisa na ukipenda kupata ushauri zaidi unaweza kuunganishwa nao.

Sura ya nane utajifunza jinsi ya kuilinda ajira na biashara yako na wakati sahihi wa kuondoka kwenye ajira. Utakapoanza biashara ukiwa kwenye ajira, siyo waajiriwa wenzako wote watafurahishwa na hilo, yatatokea majungu na fitina, hivyo unapaswa kuwa na njia ya kujilinda. Lakini pia wengi wamekuwa wanawahi kuondoka kwenye ajira zao au kuchelewa, hapa utajifunza wakati sahihi wa kuondoka.

Sura ya tisa unakwenda kujifunza mifereji nane ya kipato ambayo unapaswa kuwa nayo ili kufikia uhuru wa kifedha kwenye maisha yako. Huwezi kuwa tajiri kwa chanzo kimoja cha kipato kama mshahara pekee. Kwenye sura hii utaondoka na vyanzo vinne unavyoweza kuanza kufanyia kazi mara moja.

Sura ya kumi inakwenda kukufundisha wakati sahihi wa kuanza ni sasa na siyo kesho. Watu wengi waliingia kwenye ajira wakijiambia wataifanya kwa muda tu, lengo lao ni kuwa na biashara. Lakini wanajikuta wakiahirisha, miaka inaenda, majukumu yanaongezeka, mshahara ni kidogo, madeni ni makubwa na hawaanzi biashara zao. kwa kusoma sura ya kumi, utaondoka na hatua za kwenda kuchukua mara moja.

NYONGEZA; Kwenye kila sura ya kitabu hiki, kuna ushuhuda wa mtu aliyeanza biashara akiwa kwenye ajira, changamoto alizokutana nazo, mafanikio aliyoyapata na ushauri wake kwa wale waliopo kwenye ajira. Kwenye shuhuda hizi unakwenda kujifunza kwa watu waliokuwa wamekwama kama wewe, wakachukua hatua na sasa siyo walalamikaji tena.

Rafiki, kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA ni kitabu ambacho kila mwajiriwa anapaswa kukisoma na kuchukua hatua ili maisha yake yaweze kuwa bora zaidi.

Kitabu kinapatikana kwa nakala ngumu (Hardcopy) na bei yake ni tsh elfu 20 (20,000/=), ila kwa sababu wewe ni rafiki yangu na napenda sana upate kitabu hiki, utaweza kukipata kwa bei ya zawadi kama utakinunua kabla ya tarehe 31/10/2019. Bei ya zawadi itakuwa tsh elfu 15 (15,000/=).

Kupata kitabu hiki cha BIASHARA NDANI YA AJIRA, piga simu au tuma ujumbe kwenda namba 0678 977 007 au 0752 977 170. Kama upo Dar es salaam utaletewa kitabu popote ulipo, kama upo mkoani utatumiwa kwa njia ya basi.

Rafiki yangu mpendwa, chukua hatua sasa upate kitabu hiki kwa bei ya zawadi, na uweze kutoka hapo ulipokwama kwa sasa kwa upande wa kipato. Pia kama utahitaji ushauri zaidi wa jinsi ya kuanza na kukuza biashara yako, nunua kitabu na ukisome ukishamaliza tuwasiliane. Sipendi kukuona ukilalamika wakati zipo hatua unazoweza kuchukua, anza sasa kwa kusoma kitabu BIASHARA NDANI YA AJIRA na utaweza kuziona fursa nyingi zinazokuzunguka hapo ulipo na uchukue hatua.

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali. Kupata Huduma Za Ukocha Tembelea; www.amkamtanzania.com/kocha