Njia nzuri ya kufanya vitu kuwa bora ni kufanya vitu bora.
Huwa tunaona wengine wakitoa matokeo mazuri na kujiambia wamewezaje kufanya vile. Ambacho tunashindwa kuona ni kwamba watu hao wanatoa matokeo bora kwa sababu wanafanya vitu bora.
Unaona wengine wanatoa matokeo mazuri kwenye kazi yao na kujiuliza wamewezaje hivyo, jibu lipo wazi, wanachagua kufanya kazi bora, kupenda na kujali kile wanachofanya na kukifanya kwa umakini mkubwa ndiyo maana wanatoa matokeo bora.
Unaona wengine biashara zao zinakua na kufanya vizuri, unajiuliza ni siri gani wanayo. Hakuna siri, bali wanakuwa wamechagua kufanya biashara hiyo kwa ubora, kwanza kujitoa kwa ajili ya biashara zao, kuipenda na kupenda kuona maisha ya wateja wao yakiwa bora zaidi. Na hilo linawasukuma kufanya yale yaliyo sahihi kwa wateja wao, na hilo linapelekea biashara zao kuwa bora pia.
Njia nzuri ya kuzalisha matokeo bora ni kwa kuchagua kuchukua hatua bora katika kufanya kitu hicho. Hakuna zaidi ya hapo, hakuna siri, hakuna miujiza, ni kile unachofanya.
Kuna kauli maarufu huwa inasema Garbage In, Garbage Out, maana yake usilaumu matokeo unayopata, badala yake angalia kile unachoweka, ukiweka uchafu utatoa uchafu.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
Unavuna unachokipanda. Ujionavyo mtu ndivyo ulivyo.
Kumbe mafanikio yanaanza kwanza kwa kubadili unachokiona kwenye akili yako.
Alfref
LikeLike
Kabisa Alfred,
Lazima ianzie kwetu wenyewe.
LikeLike