Rafiki yangu mpendwa,
Je umewahi kujiwekea malengo au mipango fulani, pale mwanzoni ukawa na msukumo mkubwa sana wa kuchukua hatua lakini baada ya muda msukumo ule ukaisha kabisa na ukarudi kwenye mazoea yako?
Kama jibu ni ndiyo basi hongera, maana umedhibitisha kweli kwamba wewe ni binadamu. Hivi ndivyo binadamu tulivyo, huwa hatufanyi kitu kama hakuna msukumo unaotupelekea kufanya vitu hivyo.
Na msukumo upo wa aina mbili;
Kuna msukumo wa ndani, huu unaanzia ndani yetu wenyewe, pale tunapokuwa tunataka kitu hasa.
Halafu kuna msukumo wa nje, huu unatoka nje yetu, labda kwa wale wanaotuzunguka au kwenye mazingira, vinatusukuma tufanye kitu fulani.
Sasa kwa upande wa malengo na mipango, huwa tunaanza na msukumo wa ndani, kwa sababu ya shauku zetu za kutaka kupiga hatua. Changamoto ya msukumo huu wa ndani ni kwamba huwa haudumu, kadiri muda unavyokwenda, msukumo huu unazidi kupungua, na ndiyo maana baada ya muda unajikuta umeachana kabisa na malengo na mipango yako.
Ili kuendelea na malengo na mipango yako, unapaswa kuhakikisha unaongeza msukumo wa nje ili uendelee kukuchochea hata pale msukumo wako wa ndani unapokuwa umeisha.
Na kwa upande wa malengo, msukumo wa nje unakuja pale unaposhirikisha malengo yako kwa watu wengine, ambao hutaki kuwaangusha, ambao utawaahidi matokeo na siyo sababu. Unapojua kuna watu wengine wanakuangalia na hutaki kuwaangusha, basi unapata msukumo wa kuendelea kuchukua hatua hata pale msukumo wa ndani unapokuwa umeisha au unapokutana na changamoto zinazokatisha tamaa.
Rafiki, majuzi nilikuambia kwamba wakati sahihi kwako kuweka na kuanza kufanyia kazi malengo ya mwaka 2020 ni mapema kabla mwaka 2019 haujaanza.
Na nikakukaribisha kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2019 itakayofanyika novemba 3 ambapo utapata nafasi ya kuuanza mwaka 2020 mapema kabla ya wengine.

Leo nakupa manufaa mengine ya kushiriki semina hii ya KISIMA CHA MAARIFA 2019, ambayo ni kupata msukumo wa nje wa wewe kufanyia kazi malengo utakayojiwekea.
Kwenye semina hii, kila mtu atapata nafasi ya kuwashirikisha wengine lengo lake moja na kubwa kabisa analokwenda kufanyia kazi kwa mwaka mzima, ili mpaka tunapokutana tena kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2020 aweze kushuhudia ni matokeo gani ambayo ameyapata.
Na kila mwezi, kupitia kundi maalumu la semina hizi, kila mshiriki atawashirikisha wengine hatua anazoendelea kuchukua kwenye lengo aliloshirikisha.
Unapoweka wazi lengo lako kubwa kwa wengine, na unapolazimika kushirikisha maendeleo yako ya kila mwezi, utapata msukumo mkubwa wa kuchukua hatua na hata kama mambo yatakuwa magumu kiasi gani, hutakata tamaa, utaendelea na mapambano.
Hiki ni kitu kimoja kitakachokusaidia sana rafiki yangu, sana sana. Nimeona jinsi ambavyo watu wengi wameweza kufanya makubwa kwa huduma za ukocha wanazoshiriki, kwa hatua hii ya kutoa ripoti za mara kwa mara kwenye hatua ambazo mtu anachukua.
Sasa nataka nilete matokeo haya mazuri kwa wengi, kuhakikisha angalau kila mshiriki wa semina, kuna kitu cha tofauti anachokwenda kufanya kwa mwaka mzima, ambacho akikiangalia anasema haya ni matunda ya SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2019.
Rafiki yangu mpendwa, ombi langu kwako ni moja, fanya kila uwezalo, kuhakikisha unashiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2019. Hii siyo semina ya kukosa kama kweli umejitoa kwa ajili ya mafanikio yako. Usikubali kikwazo chochote kikuzuie kushiriki semina hii, kwa sababu utajikuta unapoteza mwaka mwingine usione ni hatua gani unazopiga.
Shiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2019 na mwaka wako wa mafanikio 2019/2020 utakuwa wa tofauti sana kwako, utakuwa na msukumo mwaka mzima wa kuchukua hatua za tofauti ili kupata matokeo ya tofauti.
SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA itafanyika jumapili ya tarehe 03/11/2019 jijini Dar Es Salaam. Semina itaanza saa moja kamili asubuhi mpaka saa moja kamili jioni. Itakuwa semina yenye vitu vingi sana, hivyo kwa siku nzima utajifunza na kuondoka na maarifa, nguvu na hamasa ya kupiga hatua zaidi.
Ili kushiriki semina hii unapaswa kulipa ada ya tsh laki moja (100,000/=) ambayo itachangia kwenye huduma zote zitakazopatikana kwenye siku ya semina. Malipo yanafanyika kwa njia ya mpesa; 0755 953 887 au tigo pesa/airtel money 0717 396 253. Ukishalipa tuma ujumbe wenye majina yako kamili na kwamba umelipia semina.
Mwisho wa kufanya malipo ili kupata nafasi ya kushiriki SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2019 ni tarehe 31/10/2019. Chukua hatua sasa ili upate nafasi ya kupata msukumo wa kufanyia kazi lengo lako moja kwa mwaka 2019/2020.
Naamini tutakuwa pamoja tarehe 03/11, karibu sana tuianze safari ya mafanikio 2019/2020 mapema.
Kocha.