“Each person acquires their own character, but their official roles are designated by chance. You should invite some to your table because they are deserving, others because they may come to deserve it.”
—SENECA, MORAL LETTERS, 47.15b
Kupata nafasi hii nyingine ya kuiona siku ya leo ni jambo la kushukuru sana.
Tunapaswa kushukuru kwa sababu hatujaiona siku hii kwa akili zetu au ujanja wetu. Bali ni kwa bahati pekee.
Tunapaswa kutumia vyema nafasi hii tuliyoipata, kwa kuweka vizuri vipaumbele vyetu.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.
Asubuhi ya leo tutafakari TABIA YAKO NDIYO HATIMA YAKO…
Watu wanakupima na kukuhukumu kwa tabia uliyonayo.
Kwa sasa watu hawaangalii sana umetokea wapi au umefanya nini huko nyuma, bali wanaangalia tabia uliyonayo sasa.
Hivyo kama unataka njia ya uhakika ya kukuza nafasi yako kwenye maisha, basi ni kujijengea tabia bora, tabia zenye manufaa kwa wengine.
Unapojijengea tabia kama uaminifu, uadilifu, kujituma, ujasiri, ung’ang’anizi na nyinginezo, wengine wanakuwa tayari kushirikiana na wewe.
Pia pale unapotafuta watu wa kushirikiana nao maeneo mbalimbali ya maisha yako, angalia zaidi tabia ambazo watu wanazo sasa na siyo kusikiliza maneno yao au historia ya nyuma.
Tabia alizonazo mtu sasa ndiyo kipimo sahihi kama atakufaa kwa kile unachohitaji.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kujijengea tabia bora ambazo zitawavutia watu sahihi kushirikiana na wewe. Pia tumia tabia kuchuja wale unaotaka kushirikiana nao kwenye maisha yako.
#UnapimwaKwaTabia #WapimeWengineKwaTabia #JijengeeTabiaBora
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1