Rafiki yangu mpendwa,
Kama ambavyo nimekuwa nakushirikisha kwa muda sasa, semina yetu ya KISIMA CHA MAARIFA 2019 itafanyika jumapili ya juma hili, tarehe 03/11/2019 jijini Dar es salaam.
Hii ni semina ya kipekee kwa wanamafanikio wote, watu ambao wamejitoa kweli kuhakikisha wanapiga hatua kubwa kwenye maisha yao, wanakutana pamoja, kujifunza na kuhamasika ili kuweza kuchukua hatua kubwa zaidi.
Semina ya mwaka huu 2019 itakuwa ya tofauti kidogo na za miaka ya nyuma kwa sababu kila mshiriki atajiwekea lengo moja atakalowashirikisha wengine na kulifanyia kazi mwaka mzima huku akishirikisha maendeleo yake kila mwezi.

Leo nakwenda kukushirikisha wanenaji tisa watakaoshirikisha mafunzo mbalimbali kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2019.
Karibu sana kwenye semina hii, ili uweze kujifunza, uhamasike na ukachukue hatua kubwa kwenye maisha yako zitakazokufikisha kwenye mafanikio makubwa.
- Kocha Dr Makirita Amani
Kocha Dr Makirita Amani atakuwa mnenaji mkuu kwenye semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2019. Atatoa masomo makuu mawili ambayo ni MAISHA YA MAFANIKIO na KIPATO ZAIDI 2020.
Kwenye MAISHA YA MAFANIKIO atafundisha MSINGI, MWONGOZO NA MSIMAMO wa maisha ya mafanikio tunavyopaswa kuiishi kila siku ya maisha yetu ili tuweze kupiga hatua zaidi na kutoruhusu changamoto mbalimbali zitusumbue.
Kwenye somo la KIPATO ZAIDI 2020, atafundisha msingi muhimu wa kuongeza kipato kwenye mwaka wa mafanikio 2019/2020 na kufundisha dhana moja ambayo kila mtu ataifanyia kazi na kwenye mkutano ujao atakuwa ametengeneza kipato zaidi kuliko alichotengeneza mwaka huu.
Masomo haya mawili yatakupa hatua kubwa na za tofauti za kuchukua kwa mwaka wa mafanikio 2019/2020 ili uweze kupiga hatua na kufanikiwa zaidi.
- Mwalimu Hamisi Msumi
Mwalimu Hamisi Msumi atakwenda kutufundisha kuhusu mahusiano yetu kwenye maisha na jinsi ya kuyaboresha ili kuweza kupiga hatua zaidi. Mahusiano yetu na wengine na ubora wake yana mchango mkubwa sana kwenye mafanikio yetu, yanapokuwa bora tunaweza kufanikiwa sana.
Kwenye SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2019, Msumi atatushirikisha JINSI YA KUZITAMBUA NA KUZIKABILI CHANGAMOTO KWENYE MAHUSIANO. Hakuna mahusiano yanayokosa changamoto, na usipoweza kukabili changamoto za mahusiano vizuri, huwezi kufanikiwa. Somo hili ni muhimu sana kwa kila mmoja wetu.
- Mhasibu Hafidhi Ally.
Moja ya changamoto ambazo wafanyabiashara wengi wanapitia na inayowarudisha nyuma ni kutokuzijua namba zao za kibiashara. Wengi wanaendesha biashara kwa mazoea na kutokujua wapi wanaelekea, kitu ambacho kinasababisha biashara nyingi kufa.
Mhasibu Hafidhi Ally anakwenda kutufundisha kuhusu NAMBA MUHIMU ZA BIASHARA NA JINSI YA KUZITUMIA KWA MAFANIKIO. Biashara ni mchezo wa namba, na jinsi unavyozijua vizuri namba zako na kuzifanyia kazi ndivyo unavyoweza kupiga hatua zaidi. Kila mtu anapaswa kupata somo hili la namba za biashara ili kuweza kusimamia biashara yake vizuri na kufanikiwa.
- Wakili Isaack Zake.
Wakili Isaack Zake amekuwa na huduma nzuri sana ambazo zinaweza kuwasaidia watu kwa upande wa sheria na hata mahusiano. Lakini kwa kipindi kirefu (zaidi ya miaka miwili) amekuwa akiahirisha kushirikisha huduma hizi kwa wengine. Mfano ameandika vitabu mbalimbali lakini kwa muda hajaweza kuvitoa. Mwaka huu 2019 alishiriki kwenye programu ya ukocha ya GAME CHANGERS na ndani ya siku 30 ameweza kufanya makubwa sana. Ameweza kuchapa vitabu viwili, kukamilisha kitabu cha tatu na kuanzisha huduma mpya ya kisheria kwa waajiri. Vitu hivi amekuwa anapanga kuvifanya kwa muda mrefu lakini kwa kukosa msukumo alikuwa anaahirisha.
Kwenye semina ya KISIMA CHA MAARIFA Wakili Zake atatushirikisha jinsi programu ya GAME CHANGERS ilivyomsaidia kupiga hatua kubwa ambayo hajawahi kupiga kwenye maisha yake. Lakini pia atashirikisha vitabu ambavyo ameshavitoa, ikiwepo kitabu cha ndoa kinachoitwa MIAKA 5 MAKOSA 50 na kitabu cha sheria za uajiri kinachoitwa 15 RULES OF ENGAGEMENT. Kupitia Zake na wewe utajifunza kwamba unaweza kupiga hatua kubwa.
- Mfugaji Sebastian Kalugulu
Sebastian Kalugulu ni mmoja wa watu ambao amekuwa akinishangaza kwa namna anavyoweza kufanya miradi mingi kwa wakati mmoja huku akiwa ni mwajiriwa. Wakati watu wengi wakishindwa hata kuanza biashara moja kwa kusingizia ajira zinawabana, Sebastian ni mfugaji wa kuku, mfugaji wa nguruwe, anajihusisha na biashara ya gari la kubeba mizigo na pia anapanga kujihusisha na ufugaji wa samaki kupitia vizimba kwenye ziwa victoria.
Kwenye semina ya KISIMA CHA MAARIFA, Sebastian anakwenda kutushirikisha anawezaje kuendesha miradi yote hiyo, huku pia akiwa mwajiriwa. Hapa utakwenda kujifunza kwa nini hupaswi kukubali chochote kikurudishe nyuma na unaweza kuanzia hapo ulipo sasa.
- Mkulima Godius Rweyongeza
Godius Rweyongeza ni mmoja wa vijana wa kipekee sana hapa Tanzania. Akiwa bado ni mwanafunzi wa chuo, aliweza kuanza kujihusisha na kilimo mapema kabisa kama njia ya kutengeneza kipato. Lakini pia amekuwa mwandishi kupitia blogu yake ya SONGA MBELE na ameweza kuandika vitabu mbalimbali ikiwepo kitabu chake maarufu kinachoitwa TATIZO SIYO RASILIMALI ZILIZOPOTEA.
Kwenye semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2019, Godius atatushirikisha jinsi ambavyo ameweza kufanya yote hayo huku akiwa bado ni mwanafunzi wa chuo kikuu. Mwaka huu 2019 alihitimu masomo yake ya chuo kikuu, lakini amekuwa mbele ya wengine wote kwa kuwa tayari ameshaanza kujihusisha na shughuli mbalimbali za kilimo na ujasiriamali. Kupitia Godius tunakwenda kujifunza kwamba muda, mtaji na vitu vingine tunavyovisingizia siyo vikwazo kama tutaamua kweli kupiga hatua.
- Mfanyabiashara Donard Msanga
Kupitia programu ya ukocha kwenye biashara ninayoitoa, inayoitwa LEVEL UP, kuna wafanya biashara wengi ambao wameweza kunufaika sana kwa kuwa kwenye programu hiyo. Mmoja wa wafanyabiashara hao ni Donard Msanga ambaye anafanya biashara ya vifaa vya simu Dar es salaam na Dodoma.
Donard aliingia kwenye programu ya LEVEL UP kiwa na wastani wa wateja 10 anaowahudumia kwa wiki na mauzo yakiwa ni wastani wa tsh 400,000/=. Kupitia mafunzo na msukumo wa programu hii, ameweza kupiga hatua kubwa sana. Kwa wastani, idadi ya wateja anaohudumia imefikia 50 (mara 5 ya awali) kwa wiki na mauzo yameweza kuongezeka mpaka kufikia wastani wa tsh 1,600,000/= (mara 4 ya awali) kwa wiki. Hizi ni hatua kubwa sana kuweza kuzipiga ndani ya mwaka mmoja wa kuwa kwenye programu.
Kwenye semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2019, Donard atatushirikisha jinsi alivyoweza kupiga hatua hizi, ili na wewe pia uweze kupiga hatua kubwa kwenye biashara yako.
- Mfanyabiashara Leonard Amo.
Leonard Amo amekuwa mfanyabiashara mkubwa wa vocha na huduma za kifedha kupitia mitandao ya simu kwa zaidi ya miaka kumi sasa. Lakini amekuwa na changamoto mbili kubwa ambazo zilikuwa zinamzuia kukua zaidi kwenye biashara yake. Changamoto ya kwanza ilikuwa ni hasara kubwa ambayo ilikuwa inatokea kwenye biashara kila mwezi. Changamoto ya pili ilikuwa kufungua ofisi mpya na kuongeza wafanyakazi kwenye biashara yake. Alikuwa akiweka pembeni changamoto hizi mpaka pale alipoona hawezi tena kuzivumilia.
Mwezi juni 2019 alishiriki programu ya GAME CHANGERS na kuweza kuzifanyia kazi changamoto hizo kubwa za biashara yake. Kutokana na mafunzo na msukumo wa programu hiyo, ameweza kufungua ofisi mpya na kuajiri wafanyakazi wapya wawili na pia kutengeneza ongezeko la kipato kwa zaidi ya tsh 3,000,000/= kwa mwezi baada ya kuacha kufanya kwa mazoea.
Kwenye semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2019, Leonard atatuonesha kwamba pale tulipo sasa, tuna fursa kubwa za ukuaji kama tukiacha kufanya kwa mazoea na kuweka juhudi zaidi.
- Mfanyabiashara Mary Kunena.
Kwenye KISIMA CHA MAARIFA tuna hazina kubwa ya kuwa na wanawake ambao ni wapambanaji mno, ambao wanafanya mambo makubwa sana ukilinganisha na wengine katika nchi yetu. Wapo ambao wanafanya biashara kubwa za kusafiri kwenda nje ya nchi na kuleta bidhaa nchini. Na wapo wengine wanaofanya biashara za ndani ya nchi au maeneo waliyopo.
Kwenye semina ya KISIMA CHA MAARIFA 2019, tunakwenda kujifunza kutoka kwa mmoja wa wanamama hao, Mary Kunena, ambaye atatushirikisha jinsi alivyoweza kuanzisha biashara yake akiwa bado ameajiriwa. Ajira yake imekuwa inambana sana na amekutana na changamoto nyingi kwenye uendeshaji wa biashara yake, lakini hajakubali kukata tamaa, na biashara yake inakwenda vizuri sana. Kupitia Mary, tutajifunza kwa nini hatupaswi kukubali chochote kiturudishe nyuma.
Rafiki yangu mpendwa, hao ndiyo wanenaji tisa kwenye SEMINA YETU YA KISIMA CHA MAARIFA 2019, ninachoweza kusema ni kwamba hakuna semina yoyote unayoweza kuhudhuria na kukutana na timu kubwa na ya wafanyaji wa kile wanachofundisha kama SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2019. Na hawa ni wachache sana kati ya wanamafanikio wengi ambao wanafanya makubwa kwenye maeneo yao mbalimbali.
Kama utachagua kukosa SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2019, basi utakuwa umeamua kujizuia kupiga hatua wewe mwenyewe. Kwa sababu changamoto yoyote inayokukwamisha sasa, kuna watu ambao walikuwa nayo, wameweza kuivuka na wanasonga mbele. Kwa kuwa nao kwa siku nzima ya semina, utajifunza mengi sana na pia utaweza kuwauliza maswali mbalimbali na kuondoka na hatua za kwenda kuchukua ili ufanikiwe zaidi.
SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA 2019 itafanyika jumapili ya tarehe 03/11/2019 jijini dar es salaam. Semina itaanza saa moja asubuhi mpaka saa moja jioni.
Ili kushiriki semina hii, unapaswa kulipa ada ambayo ni tsh laki moja (100,000/=). Ada unalipa kupitia mpesa; 0755 953 887 au tigo pesa/ airtel money 0717 396 253. Ukishalipa ada, tuma ujumbe wenye majina yako kamili na namba ya simu na maelezo kwamba umelipia SEMINA YA KISIMA CHA MAARIFA.
Mwisho wa kufanya malipo ili kushiriki semina hii ni tarehe 31/10/2019. Zimebaki siku 3 pekee kupata nafasi hii ya kipekee sana kwako kwa mwaka wa mafanikio uliopo mbele yako. Chukua hatua sasa ili tuwe pamoja kwenye semina hii, tujifunze, tuhamasike na tukachukue hatua kubwa kwenye mwaka wa mafanikio 2019/2020.
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani.