No one has had so much divine favor
That they could guarantee themselves tomorrow.
God keeps our lives hurtling on,
Spinning in a whirlwind.”
—SENECA, THYESTES, 613
Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri tuliyoiona leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.
Asubuhi ya leo tutafakari CHOCHOTE KINAWEZA KUTOKEA…
Jambo lolote, zuri au baya linaweza kutokea wakati wowote.
Hakuna ambaye ana uhakika wa kupata mambo nzuri tu au mambo mabaya tu.
Unaweza kuwa kwenye kilele cha mafanikio na ukaanguka vibaya.
Unaweza kuwa chini kabisa na ukapata fursa ya kupanda juu na kufanikiwa.
Pamoja na juhudi kubwa tunazoweka, bado sisi siyo waamuzi wa kuu wa nini kitakachotokea au kutokutokea kwenye maisha yetu.
Hivyo yatupasa kuwa wanyenyekevu, tunapopata tusidharau na kuona nu kwa nguvu zetu, na wala tunapokosa tusikufuru na kuona tumeonewa.
Chochote kinaweza kutokea kwa wakati wowote, hivyo ndivyo dunia inavyokwenda.
Muhimu kwako ni kutumia kila ulichonacho vizuri wakati unacho na kuwa tayari kupokea chochote kinachokuja kwako na kukitumia vizuri.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuwa tayari kwa chochote kinachoweza kutokea na kukitumia vizuri.
#ChochoteKinawezaKutokea #DuniaInajiendeshaKwaMisingiYake #TumiaVizuriKilaUlichonacho
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1
Ni kweli kabisa leo asubuhi bila kutarajia nikiwa kwenye daladala nimeibiwa simu .Ni muhimu kuwa tayari kwa lolote linaloweza kutokea.Muhimu ni kuwa sahihi wakati wote lakini tutambuwe sisi sio waamuzi wa kuu wa nini kitakachotokea au kutokutokea kwenye maisha yetu.
Duuh, hili ni bonge la tafakari!!!
LikeLike
Pole sana Hafidhi kwa changamoto hiyo ya kuibiwa simu.
Vizuri umeipokea kwa namna chanya, hivyo haitakuumiza sana kama yule ambaye atalalamikia hilo wakati wote.
LikeLike