“The universe is change. Life is opinion.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 4.3.4b
Ni siku nyingine mpya, siku bora na ya kipekee sana kwetu.
Tumepata nafasi hii nzuri sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.
Asubuhi ya leo tutafakari KILA KITU KINABADILIKA…
Kila kitu hapa duniani kinabadilika,
Japo kwa nje tunaweza kuona kitu ni kile kile, lakini kila kitu kinabadilika.
Tukianza na miili yetu wenyewe, imekuwa inabadilika kila siku.
Kucha zako zinaota kila siku, unazikata zinaota tena.
Kadhalika nywele zako, kila siku zinaota zaidi. Seli za mwili wako pia zinabadilika.
Watu wengine nao wanabadilika.
Viumbe wengine nao wanabadilika.
Na dunia kwa ujumla, inadabilika.
Hivyo mambo yanapokuwa tofauti na tulivyotegemea, tusiumie, kwa sababu kila kitu kinabadilika.
Kwa kujua kwamba kila kitu kinabadilika, tunaweza kujipanga vizuri na kuyatumia mabadiliko hayo kwa manufaa kwetu.
Maisha hayasimami, dunia haisimami hivyo na wewe usisimame.
Badilika kadiri mazingira yanayokuzunguka yanavyobadilika na hapo utaweza kuziona na kuzitumia vizuri fursa zinazokuzunguka.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kwenda vizuri na mabadiliko yanayotokea kwenye kila eneo na kila kitu, kuyatumia vizuri mabadiliko hayo na kutengeneza matokoe bora kwako.
#KilaKituKinabadilika #UsiendeKwaMazoea #JaribuVituVipyaKilaSiku
Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.amkamtanzania.com/makirita3.1