Kuna wakati watu huwa wanakwama kupiga hatua, siyo kwa sababu hawana cha kufanya, ila wana vitu vingi wanavyoweza kufanya na hawajui kipi waanze nacho.
Kila wanapolinganisha vitu wanavyoweza kufanya, wanaona vyote vina umuhimu. Wakiangalia kimoja, wanagundua kingine nacho ni bora zaidi, na kingine tena.
Kinachotokea ni unakuta mtu ana vitu vingi anavyoweza kufanya, lakini hakuna anachofanya. Wengi wanakwama kwa sababu hawajui kipi bora kabisa kwao kufanya. Na wanaogopa kuanza na chochote kwa kufikiria labda huko mbele watagundua hicho walichochukua siyo bora kama vile ambavyo wamevianza.
Sasa rafiki najua unajua vizuri kabisa ya kwamba hutafanikiwa kwa kufikiria ni kipi sahihi kufanya, bali utafanikiwa kwa kuchagua kitu na kufanya.
Hivyo basi, acha sasa kufikiria ni kipi sahihi zaidi kufanya na chagua kimoja kati ya vingi unavyoweza kufanya na anza kufanya.
Hakuna fursa iliyo sahihi au isiyo sahihi, bali baadhi ya fursa zina manufaa kuliko nyingine, lakini huwezi kujua kwa kufikiria na kulinganisha. Utajua kwa kuchagua fursa yoyote kati ya nyingi zinazokuzunguka na kuanza kufanya.
Badala ya kusubiri kupata fursa sahihi, chagua fursa yoyote na ifanye kuwa sahihi kwako, kwa kuijua kwa undani na kuweka kazi ya kutosha.
Chagua moja na weka kazi, usipoteze muda kujiuliza kipi sahihi, chagua kimoja na kifanye kuwa sahihi kwako.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
Ninachofanya ndio sahihi nitakiboresha Kila siku, asante na siku njema kocha.
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike