Ndiyo mgodi wa dhahabu kwako kuweza kukua na kufanikiwa zaidi kwenye maisha yako.
Kila mtu ana wateja ambao tayari anao sasa, hata kama hayupo kwenye biashara.
Kuna watu wanaokuamini kwa kitu fulani unachofanya, hata kama hawakulipi kwa wewe kufanya kitu hicho. Hao ndiyo wateja ulionao sasa.
Na hao ndiyo unaoweza kuwatumia kupiga hatua na kufanikiwa zaidi.
Na namna ya kufanya hivyo ni rahisi, wekeza muda na nguvu zako katika kuandaa bidhaa au huduma bora kwa watu hao wanaokuamini, kisha kazana kutoa huduma bora kabisa kwa wateja hao na kisha watumie hao kupata wateja zaidi.
Jambo hili linahitaji kazi na linahitaji muda pia, lakini ni uwekezaji ambao ukiufanya utakunufaisha sana.
Hatua muhimu ya kuchukua ni kujiuliza ni wateja gani ulionao sasa, ni watu gani wanaokuamini sana kwenye chochote kile unachofanya, wajue kwa undani na kisha wekeza katika kuwaandalia kilicho bora kwao, wape huduma bora na watumie hao kuwafikia watu wengi zaidi.
Hapo ulipo tayari unao wateja wa aina hiyo, kazi ni kwako kuwatambua, kuwahudumia na kisha kuwatumia kuwafikia wengi zaidi.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
Asante kocha ,ni kweli nina watu waniamini sana kwa mambo ninayofanya nitazidi kutumia hao kupata wateja zaidi
LikeLike
Vizuri sana.
LikeLike