“Think of the life you have lived until now as over and, as a dead man, see what’s left as a bonus and live it according to Nature. Love the hand that fate deals you and play it as your own, for what could be more fitting?”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 7.56–57

Hongera mwanamafanikio kwa kuiona siku hii nyingine nzuri ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kusimamia maeneo hayo matatu, siku ya leo itakuwa bora sana kwetu.

Asubuhi ya leo tutafakari CHEZA KARATA ULIZOPEWA…
Kama umewahi kucheza mchezo wa karata, unajua kabisa kwamba unapewa karata bila ya kujua ni za aina gani.
Na ili mchezo uende, unapaswa kucheza karata ulizonazo, hata kama siyo karata nzuri za kukuwezesha kupata ushindi.
Hivyo pia ndivyo maisha yalivyo, kila siku tunayoiona ni sawa na karata ambazo tumepewa.
Ili maisha yaweze kwenda, jukumu letu kuu ni kuzicheza karata, kuiishi kila siku kwa ukamilifu wake.

Kila siku inakuja kwako na mambo yake, na siyo yote ambayo utakuwa unayapenda.
Lakini huna budi kuiishi kila siku yako vyema, iwe yanayotokea unayapenda au la.
Na kumbuka, hutakuwa na siku nyingine kama hii maishani mwako, hivyo iishi siku hii vyema.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuiishi leo kama ambavyo imekuja kwetu na kutumia kila hali kuishi vyema.
#MaishaNiMchezo #UchezeKwaUkamilifu #HutapataSikuNyingineKamaLeo

Wako rafiki katika safari ya kuelekea mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania