“This is the mark of perfection of character—to spend each day as if it were your last, without frenzy, laziness, or any pretending.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 7.69
Kuiona siku hii mpya ya leo ni jambo la kushukuru sana.
Kwa sababu ni bahati ambayo tumeipata sisi wachache,
Wapo wengi waliopenda kuipata na wangekuwa tayari kulipa gharama kubwa ili tu waione leo, lakini hawajapata nafasi hii.
Hivyo kushukuru na kuiishi siku hii vizuri ndiyo njia pekee ya kuitumia zawadi hii ya leo.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Na msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kuzingatia maeneo hayo matatu, siku hii ya leo itakuwa bora na ya kipekee sana kwetu.
Asubuhi ya leo tutafakari NJIA RAHISI YA KUPIMA KILA SIKU YAKO…
Alama ya tabia iloyotukuka ni kuishi kila siku yako kama vile ndiyo siku ya mwisho kwako hapa duniani, bila ya uvivu, kuahirisha mambo au kujifanya haujui mwisho ni lini.
Kufikia ukamilifu kama mwanadamu ni kitu kigumu, lakini kukazana kila siku kusogea karibu zaidi na ukamilifu ni kitu kinachowezekana.
Na njia ya kufanya hivyo ni kuichukulia kila siku yako kama ndiyo siku ya mwisho kwako kuwa hai.
Kama leo ni siku yako ya mwisho, hakika hutaipoteza kulalamika, kufuatilia wengine, kugombana, kuwa na chuki na mtu mwingine au kuahirisha yale muhimu.
Sasa kwa nini uendelee kuyafanya hayo?
Kuna mtu amekupa mkataba wa kukuhakikishia kesho utakuwepo?
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuishi kama vile ndiyo siku ya mwisho kwako kuwa hapa duniani na hivyo kuishi vizuri na kufanya yale yaliyo sahihi.
#HutaishiMilele #HuendaLeoNdiyoMwisho #FanyaKilichoSahihi
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania
Asante kocha kila siku nitatumia hiyo kauli ili niweze kuitumia vizur siku yangu.
LikeLike