“Both Alexander the Great and his mule-keeper were both brought to the same place by death—they were either received into the all-generative reason, or scattered among the atoms.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 6.24

Hongera mwanamafanikio kwa siku hii nyingine nzuri sana ya leo.
Ni nafasi bora na ya kipekee sana kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo makubwa sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Na msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kuzingatia maeneo hayo matatu, siku hii ya leo itakuwa bora na ya kipekee sana kwetu.

Asubuhi ya leo tutafakari KITU KIMOJA KINACHOTULINGANISHA WOTE…
Maisha yanaweza kujenga matabaka mbalimbali baina ya binadamu,
Kuja matajiri na masikini,
Viongozi na wafuasi,
Wenye ushawishi na wasio na ushawishi,
Watu mashuhuri na watu wa kawaida,
Na kadha wa kadha.

Lakini matabaka yote hayo ni ya muda tu,
Kuna kitu kimoja kinachotusubiri wote, ambacho kinatulinganisha.
Kitu hicho hakiruhusu matabaka baina ya watu.
Kitu hicho ni kifo.
Kifo kinakuja sawa kwa wote na baada ys kifo watu wote wanalingana.
Hakuna tena matabaka baada ya kifo, wote ni wafu.

Ni muhimu sana kujikumbusha hili ili uwe mnyenyekevu,
Pale unapojiona ni muhimu kuliko wengine jikumbushe kifo kitawaweka sawa tu.
Na hata pale unapojiona uko chini zaidi ya wengine, unapokata tamaa ukiangalia mambo ya wengine, jikumbushe kwamba kifo hakitamwacha hata mmoja.

Lengo la kujikumbusha hili siyo kuwa mvivu na kuishi kizembe, badala yake kuishi kwa kusudi na kutoruhusu kiburi au uvivu ukitawale.
Kwa sababu unajua wote tunakuja kulinganishwa na kifo.

Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kukukumbuka kwamba kifo kinatulinganisha wote, hivyo kuwa mnyenyekevu na kufanya kilicho sahihi mara zote.
#KifoHakinaMatabaka #UsijilinganisheNaWengine #FanyaKilichoSahihi

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani
http://www.t.me/somavitabutanzania