“Think of the whole universe of matter and how small your share. Think about the expanse of time and how brief—almost momentary—the part marked for you. Think of the workings of fate and how infinitesimal your role.”
—MARCUS AURELIUS, MEDITATIONS, 5.24
Ni siku mpya, siku nzuri na ya kipekee sana kwetu.
Tumeipata nafasi bora kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kuweza kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kuzingatia maeneo hayo matatu, siku hii ya leo itakuwa bora na ya kipekee sana kwetu.
Asubuhi ya leo tutafakari KIPIMO CHAKO KWENYE DUNIA…
Ukiichukua dunia, halafu ukajilinganisha na wewe, unakuwa mdogo mno hapa duniani.
Ukiangalia ukubwa wa dunia, ukilinganisha na ukubwa wako, wewe ni kama sisimizi tu.
Ukiangalia umri ambao dunia imekuwepo na kulinganisha na umri ambao wewe utaishi hapa duniani ni kama unapita kwa sekunde tu.
Kujilinganisha huku na dunia kunakufanya uielewe nafasi yako sahihi kwenye hii dunia.
Kwa sababu kuna wakati tunajisahau, na kuanza kuona kama vile tunaidai dunia kitu, na kuanza kulalamika kwa mambo ambayo tungepaswa kuyashukuru.
Kwa kutambua nafasi yako sahihi kwenye dunia, itakisaidia kufikiri kwa usahihi na kuchukua hatua sahihi.
Utaacha kuilalamikia dunia kwa lolote lile na kushukuru kwa kila nafasi ambayo unaipata, kwa sababu ni upendeleo kwako.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kuangalia ulinganisho wako na dunia na kuitambua nafasi sahihi kwako ni ipi.
#DuniaNiMuhimuKukikoWewe #DuniaUmeikutaNaUtaiacha #KuwaMnyenyekevu
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani
http://www.t.me/somavitabutanzania
Asante kocha kweli dunia nikubwa kuliko Mimi, na hakuna kitu ambacho naidai dunia , nimeikuta na nitaicha kwahiyo nifanye yale yaliyo sahihi kwa muda huu ninaopita hapa duniani.
LikeLike