“The mind must be given relaxation—it will rise improved and sharper after a good break. Just as rich fields must not be forced—for they will quickly lose their fertility if never given a break—so constant work on the anvil will fracture the force of the mind. But it regains its powers if it is set free and relaxed for a while. Constant work gives rise to a certain kind of dullness and feebleness in the rational soul.”
—SENECA, ON TRANQUILITY OF MIND, 17.5
Ni siku nyingine mpya, siku bora na ya kipekee sana kwetu.
Tumeiona nafasi hii nyingine nzuri kwetu kwenda kuweka juhudi kubwa ili kupata matokeo bora sana.
Msingi wetu ni NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA,
Mwongozo wetu ni AFYA, UTAJIRI NA HEKIMA,
Msimamo wetu ni KAZI, UPENDO NA HUDUMA.
Kwa kuzingatia maeneo hayo matatu, siku hii ya leo itakuwa bora na ya kipekee sana kwetu.
Asubuhi ya leo tutafakari MAPUMZIKO NI MUHIMU…
Shamba lenye rutuba likilimwa kwa muda mrefu bila ya kupumzishwa, rutuba yake huisha na uzalishaji wake hupungua sana.
Hivyo pia ndivyo miili yetu ilivyo, ikifanyishwa kazi kwa muda mrefu bila kupumzishwa huchoka haraka na ufanisi hupungua.
Kadhalika akili zetu, zikifanyishwa kazi muda mrefu bila ya mapumziko zinachoka na uwezo wa kufanya maamuzi unapungua.
Pamoja na mipango mikubwa unayoweza kuwa nayo, njia pekee ya kukuwezesha kuifikia ni kupata muda wa kupumzika.
Pamoja na uhitaji mkubwa wa kufanya kazi kwa muda mrefu, njia pekee ya kukuwezesha kufanya hivyo ni kuwa na muda wa kupumzika.
Hakikisha kwenye utaratibu wako wa kila siku umetenga muda wa kupumzika.
Huo ndiyo muda wa kuchaji mwili na akili yako, ili viwe na nguvu ya kuendelea na mapambano.
Ukawe na siku bora sana ya leo, siku ya kutenga muda wa kupumzisha mwili na akili yako ili viweze kupata nguvu mpya na uweze kuwa na ufanisi mzuri.
#MapumzikoNiMuhimu #KisichopumzikaKinavunjika #HataBetriYaSimuHuchajiwa
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania