Habari rafiki yangu mpendwa?

Napenda kuchukua nafasi hii kukuletea salamu za sikukuu ya Krismasi na Mwaka mpya 2020.

Kipindi cha sikukuu ni wakati mzuri wa kuwa pamoja na wale watu wa muhimu kwetu, ambao wakati mwingine hatupati nafasi nzuri ya kuwa nao.

Hivyo nikutakie heri na utulivu katika kipindi hiki, ili uweze kupata mapumziko na kuimarisha mahusiano yako pia.

Pia nikusihi katika kipindi hiki kupata muda wa kuyatafakari maisha yako, unakotoka, ulipo na kule unapokwenda, ili uweze kujua hatua sahihi kwako kuchukua.

Kipekee sana nikushukuru kwa kipindi chote ambacho tumekuwa pamoja kwenye safari hii ya kujifunza na kupiga hatua ili kufanikiwa.

2020...jpg

Wewe umekuwa sababu ya mimi kujituma na kujisukuma kila siku. Bila ya uwepo wako mimi siwezi kupiga hatua. Na kama ambavyo nimewahi kukushirikisha falsafa kuu ninayoendesha nayo huduma zangu, mafanikio yangu ni mafanikio yako. Ili mimi nifanikiwe basi inabidi wewe ufanikiwe kwanza. Na ndiyo maana naweka nguvu kubwa sana kuhakikisha wewe unafanikiwa, kwa sababu ukishafanikiwa wewe, na mimi nitafanikiwa.

Kama ambavyo nimekuwa nakushirikisha mara kwa mara, safari hii ya kujifunza ili kufanikiwa haina ukomo, haina kuhitimu, kila siku mpya ni nafasi mpya ya kujifunza na kuchukua hatua mpya. Hivyo naamini tutaendelea kuwa pamoja kwenye safari hii kwa wakati wote ambao kila mmoja wetu atakuwa hai.

Kuna vitu vitatu ambavyo nimejiambia nitavifanya kila siku ya maisha yangu, yaani ninapoamka tu na nikawa na pumzi siku hiyo, lazima nivifanye vitu hivyo vitatu. Vitu hivyo ni KUANDIKA, KUSOMA na KUKOCHI. Kama unavyoona, vitu hivyo vitatu vinategemea sana uwepo wako, hivyo naamini tutaendelea kuwa pamoja kwenye safari hii.

Nikuahidi kwamba mwaka 2020 na kuendelea nitaendelea kukushirikisha maarifa bora yenye hatua za kuchukua ili uweze kufanikiwa zaidi. Naamini sana kwenye maarifa na kuchukua hatua, vitu viwili ambavyo ukivifanyia kazi basi utaweza kupiga hatua sana.

Mafunzo yote ya mafanikio yataendelea kupatikana kwenye mitandao miwili, AMKA MTANZANIA (www.amkamtanzania.com) na KISIMA CHA MAARIFA (www.kisimachamaarifa.co.tz) Kila siku tembelea mitandao hii miwili na kutakuwa na makala na mafunzo mazuri kwa ajili ya mafanikio yako.

Mwaka 2020 nitakwenda kuweka nguvu kubwa zaidi kwenye usomaji na uchambuzi wa vitabu. Baada ya kufanya hili kwa muda, nimeona lina nguvu kubwa ya kuwabadili wengi, lakini wengi hawalipi uzito. Hivyo mpango ambao nafanyia kazi sasa ni kufikia watu 1000 kwenye channel ya SOMA VITABU TANZANIA. Hii ni channel ambayo ipo kwenye mtandao wa telegram na ambayo inakupa vitabu pamoja na chambuzi zake. Kitu cha ziada kitakachopatikana kwenye channel hii ni mafunzo ya JINSI YA KUSOMA KITABU na MAISHA YA WABUNIFU. Huu ni uchambuzi ambao utafanyika kila wiki na utakusaidia sana kuweza kusoma na kuelewa na hata kutengeneza utaratibu mzuri kwako kuendesha maisha yako. Kama bado hujajiunga na channel ya SOMA VITABU TANZANIA, fungua kiungo hiki kujiunga sasa; https://www.t.me/somavitabutanzania

KISIMA CHA MAARIFA mwaka 2020 kinakwenda kuwa tofauti kidogo, kwanza kabisa nafasi za kuwa mwanachama zinakwenda kuwa chache na ninakwenda kufanya kazi na watu wachache waliojitoa kweli kwa ajili ya kufanikiwa. Nimekuwa naweka nguvu kubwa sana kwenye huduma hiyo lakini kuna ambao wamekuwa hawaipi uzito. Hivyo nakwenda kuwapunguza wale ambao hawaipi uzito huduma hiyo, wale ambao hawachukui hatua sahihi za kuyafanya maisha yao kuwa bora zaidi. Hivyo kama ni mwanachama tayari unapaswa kuchukua hatua ili kuendelea kuwa mwanachama. Na kwa wale ambao bado hawajawa wanachama na wanapanga kuwa wanachama unahitaji kujitoa kweli ili kupata nafasi hiyo.

Huduma nyingine za ukocha za GAME CHANGERS na LEVEL UP zinaendelea kupatikana kwa wanachama wa KISIMA CHA MAARIFA.

Vitabu mbalimbali vya mafanikio vinaendelea kupatikana, kama ELIMU YA MSINGI YA FEDHA, BIASHARA NDANI YA AJIRA na TANO ZA MAJUMA 50 YA MWAKA. Mwaka 2020 tutachapa vitabu vingine pia na taarifa zitatolewa kupitia mitandao yetu. Kupata vitabu wasiliana na namba 0678 977 007 au 0752 977 170.

Rafiki, naamini tutaendelea kuwa pamoja kwenye huduma hizi kwa mwaka 2020 na kuendelea. Nimejitoa kwa ajili yako, naamini naweza kupata chochote ninachotaka kama nitawasaidia wengi zaidi kupata kile wanachotaka. Hivyo karibu sana twende pamoja katika safari hii isiyokuwa na mwisho. Chagua huduma ambayo tutakuwa pamoja katika hizi nilizokushirikisha.

Nina ombi moja muhimu sana kwako rafiki yangu, sambaza ujumbe huu kwa marafiki zako ili nao wapate fursa ya kunufaika na maarifa haya. Hii itakuwa ni moja ya zawadi kubwa sana utakayokuwa umewapa kwenye msimu huu wa sikukuu. Kama umepokea kwa barua pepe, itume kwa wengine, kwenye wasap tuma kwa wengine pia.

Asante sana rafiki yangu, uwe na wakati mwema kwenye msimu huu wa sikukuu na usiache kukazana kuwa bora kwenye kila siku mpya unayoipata.

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,

Kocha Dr Makirita Amani.