“The most important question to keep before ourselves at all times is this: Do we do the right thing? During this short period of time which we call our life, do our acts conform to the will of the force that sent us into the world? Do we do the right thing?” – Leo Tolstoy
Upo hapa duniani kwa kusudi maalumu,
Haupo hapa kwa bahati mbaya.
Hivyo wajibu wako ni kulijua kusudi lako na kuliishi kila siku.
Kila siku fanya kilicho sahihi katika kuliishi kusudi lako.
Ukishafanya kilicho sahihi, mengine yote yatakaa sawa yenyewe.
Unapoimaliza kila siku yako jiulize je umefanya kilicho sahihi?
Pitia siku yako nzima kwa kila ulichofanya na jiulize kama ulichofanya ni sahihi na umekifanya kwa usahihi.
Kwa yale ambayo hukufanya kwa usahihi leo, nenda kayafanye kwa usahihi kesho.
Na kila unapokuwa njia panda, kila unapokuwa na wasiwasi na hujui ufanye nini, fanya kilicho sahihi.
Kama ambavyo Mstoa Marcus Aurelius amewahi kusisitiza; “Just that you do the right thing. The rest doesn’t matter.”
Tukazane kufanya kilicho sahihi, na mengine yote yatajipanga yenyewe.
Ukawe na wakati mwema, ukiwa na maandalizi bora kwa siku ya kesho.
Kocha.