“Even if we don’t want to, we can’t help but feel our connection to the rest of mankind: we are connected by industry, by trade, by art, by knowledge, and most importantly, by our common mortality.” –
Leo Tolstoy

Hata kama hatutaki, binadamu wote ni kitu kimoja.
Tuna vitu vingi vinavyotuleta pamoja kuliko vinavyotutenga.
Tunaletwa pamoja na biashara mbalimbali zinazotupa mahitaji yetu.
Tunaletwa pamoja na taalumu mbalimbali tulizonazo, ambazo zinategemeana.
Tunaletwa pamoja na elimu na hata maarifa mbalimbali tunayoyapata na kuyatumia.
Na muhimu zaidi, mwisho wetu ni mmoja, ambao ni kifo. Wote tunawekwa sawa na kifo, kwa kuwa hakuna atakayekikwepa.

Kwa kujua namna tunavyoletwa pamoja na vitu vilivyo vingi tunaona umuhimu wa kushirikiana kuliko kutengana.
Kwa sababu kwa kushirikiana wote tunanufaika zaidi.

Unapoimaliza siku yako ya leo, tafakari ni kwa namna gani umeweza kushirikiana na wengine leo, hi vipi umeweza kujenga na kuboresha mahusiano yako na wengine.
Na kesho, nenda kaweke juhudi zaidi katika kushirikiana na wengine na kuboresha mahusiano yako.

Uwe na wakati mwema.
Kocha.