When you hear people speak about the viciousness of other people, do not share in pleasure by discussing these issues. When you hear about the bad deeds of people, do not listen to the end and try to forget what you have heard. When you hear about the virtues of other people, remember them and tell them to others. — EASTERN WISDOM

Hongera sana kwa kuiona siku hii nyingine mpya na nzuri sana ya leo.
Karibu kwenye tafakari ya kwenda kuianza siku hii kwa mtazamo sahihi na kufanya kilicho sahihi.

Unaposikia watu wakijadili mabaya ya mtu mwingine, usijiunge nao na kushiriki mazungumzo hayo.
Unapokuta watu wanajadili mauvu ya wengine, usisikilize na kujiambia utaachana nayo.
Epuka kabisa kushiriki mazungumzo ambayo mtu mwingine anasemwa kwa ubaya, na yeye hayupo.
Hata kama yanayosemwa ni kweli, mazungumzo ya aina hiyo hayana manufaa kwa wanaosema na hata anayesemwa.
Lakini yana hatari ya kile kilichosemwa kumfikia mlengwa na kikazua mgogoro au hali ya kutokuelewana.

Unaposikia wengine wakimjadili mtu kwa mambo mazuri, hayo yakumbuke na yasambaze kwa wengine pia.
Lakini yale mabaya usishiriki na chochote kibaya unachokuwa umekisikia sahau kabisa.
Jiepushe sana kuwa sehemu ya majungu au kuwasema wengine vibaya, haya kama yanayosemwa ni kweli.
Kama kweli unataka kumsaidia mtu, basi mkabili waziwazi ukimweleza uhalisia wa hali aliyonayo.
Lakini kukaa na wengine kusema mabaya ya asiyekuwepo ni majungu yasiyo na manufaa yoyote.
Na chochote utakachochangia, jua kitasambaa na kueleweka kwa namna ambayo hukukusudia.

Jijengee msingi rahisi, weka pamba masikioni na zipo mdomoni inapokuja kwenye mabaya ya wengine.
Na kuwa msikivu na msemaji mzuri inapokuja kwenye mazuri ya wengine.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania