Hizi ni hatua tatu ambazo ni muhimu sana kuzifanyia kazi kwenye kila eneo la maisha yetu.
Tukianza na maisha yetu wenyewe, tunapaswa kuyatengeneza, kuyatunza na kisha kuyakuza zaidi.
Kwenye fedha, tunapaswa kutengeneza kipato, kukitunza na kisha kukikuza zaidi.
Kwenye mahusiano, tunapaswa kuyatengeneza, kuyatunza na kisha kuyakuza zaidi.
Watu wengi wanashindwa kwa sababu kuna hatua wanairuka au kuipuuza katika hizo tatu.
Wengi wanakazana kutengeneza mahusiano, lakini baada ya hapo hawahangaiki kuyatunza, na hilo linapelekea mahusiano hayo kuvunjika.
Kadhalika wengi wanakazana kutengeneza kipato, wanafanya kazi sana ili wapate fedha sana, lakini hawazitunzi, badala yake wanatumia zote, na hivyo kila wakati wanajikuta wakilazimika kutengeneza upya fedha zao. Au mtu anatengeneza na kutunza fedha, lakini hazikuzi, hivyo anachotunza kinaishia kupotea au kupoteza thamani.
Kwenye kila eneo la maisha yako, zingatia mambo haya matatu, tengeneza, tunza, kuza.
Angalia popote ulipokwama sasa na utaona kuna mahali ambapo labda hutengenezi, hutunzi au hukuzi zaidi.
Kila siku jiulize ni nini unaenda kutengeneza, kutunza na kukuza kwenye kila eneo la maisha yako, na kwa kufanyia kazi maeneo hayo matatu utaweza kuwa na maisha bora sana.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
Ahsante sana kocha kwa ujumbe huu wa ukurasa wa Leo. Nimependa sana kanuni hii,” tengeneza,tunza na kuza” hii kweli ni halisi kwenye maisha yetu.
LikeLike
Karibu.
LikeLike
Asante kocha , kila siku nitatumia maeneo hayo matatu kutengeneza, kutunza na kukuza.
LikeLike
Asante sana, kuazia sasa nitatumia haya maeneo matatu kwa kila jambo ninalolifanya, kutengeneza, kutunza na kukuza
LikeLike