“The basis of all education is the establishment of our relationship to the beginning of all things, and the conclusions about our behavior which may be drawn from this.” – Leo Tolstoy

Msingi mkuu wa elimu ni kujitambua sisi wenyewe na kujua uhusiano wetu na dunia pamoja na asili.
Kujua jinsi ambavyo kile tunachofanya kinaathiri kila kitu kwenye hii dunia.
Kujua ya kwamba ushirikiano wetu na wengine ndiyo njia pekee ya kuifanya dunia kuwa sehemu bora.
Kama elimu unayopata haikujengi kwenye misingi hii, hiyo siyo elimu sahihi kwako.
Kama elimu na malezi unayotoa kwa wengine hayawajengi kwenye msingi huo unawapoteza.

Unapoimaliza siku ya leo, jiulize ni kwa namna gani uliyojifunza leo na uliyofundisha leo yapo kwenye msingi sahihi.

Ukawe na wakati mwema na unapoianza kesho, uianze kwa msingi sahihi.
Kocha.