“The higher the position you occupy among other people, the more humble you should be. Many people live in height and glory, but the mysteries of this world can be revealed only to those who are humble. Do not seek out complication. Treat your duty with respect. Do not study what you should not. More things have already been revealed to you than you can understand.” —From APOCRYPHA

Tumeiona siki hii nyingine mpya na ya kipekee sana kwetu.
Nafasi hii tuliyoipata ni kwa bahati, hivyo kushukuru na kuitumia siku hii vizuri ndiyo kitu pekee tunachopaswa kufanya.

Kadiri unavyopanda juu, kadiri unavyofanikiwa, kadiri unavyopanda cheo, basi unapaswa kuwa mnyenyekevu zaidi.
Watu wengi wanaishi kwenye ukuu na mafanikio, lakini siri za dunia zinafunuliwa kwa wale ambao ni wanyenyekevu.

Usiyafanye mambo kuwa magumu kuliko yalivyo.
Tekeleza majukumu yako kwa usahihi.
Na usihangaike na yale yasiyokuhusu, kwa sababu tayari una mengi ambayo tayari yameshafunuliwa kwako ambayo bado hujayaelewa.

Hadithi ya aina hii huwa inajirudia kila wakati, mtu anaanzia chini kabisa, anakuwa mnyenyekevu na unyenyekevu huo unamwezesha kupiga hatua na kufanikiwa au kupanda cheo.
Kadiri anavyopanda, unyenyekevu unazidi kupungua, kiburi na ujuaji vinaanza kukua.
Na pale unyenyekevu unapoisha kabisa na kiburi na majivuno kutawala, ndipo wengi huanguka vibaya licha ya kuwa wamefika juu kimafanikio au kiuongozi.

Usikubali hadithi hii itokee kwako au kama ilishatokea basi usikubali ijirudie.
Kuwa mnyenyekevu.
Kadiri unavyopiga hatua, ndani yako utaanza kuona kwamba umeshajua kila kitu.
Kadiri watu wanavyokusifia kwa hatua unazopiga, ni rahisi kuona tayari umeshamaliza kila kitu.
Lakini huo ndiyo wakati wa kuwa makini na kujilazimisha kuwa mnyenyekevu.

Kwa kuwa mnyenyekevu unaendelea kujifunzam unaendelea kushirikiana na wengine na kuendelea kujituma kama awali.
Kwa kuwa na kiburi unaona huna kipya cha kujifunza, unaona wengine wote wako chini yako na huwahiyaji na hujitumi tena kama awali.
Ndiyo maana wanyenyekevu wanazidi kufanikiwa na kufikia ukuu, huku wenye kiburi na majivuno wakianguka vibaya.

Kuwa mnyenyekevu, ndiyo njia pekee ya kudumu kwenye mafanikio.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania