“When an arrow does not hit its target, the marksman blames himself, not another person. A wise man behaves in the same way.” —CONFUCIUS

Mshale unapokwenda nje ya lengo, mlengaji hana wa kumlaumu isipokuwa yeye mwenyewe.
Hivyo ndivyo wenye hekima wanavyoyaendesha maisha yao,
Wanajua chochote kinachotokea kwenye maisha yao, hawana wa kumlaumu, bali wao wenyewe.

Hivyo ndivyo tunavyopaswa kuyaendesha maisha yetu,
Tunapokosa kile tulichotaka, tusianze kutafuta wa kumlaumu, bali tuangalie tulikosea wapi na kufanya marekebisho.
Ukiweza kuyaendesha maisha yako bila ya kumlaumu yeyote, utapunguza sana msongo kwenye maisha yako.

Tukawe na wakati mwema, na kesho ikawe siku ya kubeba jukumu la maisha yetu na makosa yetu bila ya kumlaumu yeyote.

Kocha.