“If you don’t make mistakes, you’re not working on hard enough problems. And that’s a big mistake.” —FRANK WILCZEK

Kama hujawahi kushindwa au kukosea kwenye jambo lolote unalofanya, siyo kwamba wewe ni mjanja sana, bali hujajaribu vitu vikubwa.
Umekuwa unafanya vitu ambavyo umezoea kufanya.
Na hilo ni kosa kubwa sana, kwa sababu kama hujaribu vitu vipya na vikubwa basi haupo kwenye nafasi nzuri ya kupiga hatua na kufanikiwa.

Usifurahie kutokufanya makosa, badala yake jiulize kipi cha tofauti ulichokaribu kufanya, kama hakuna, basi jua unajipoteza.
Kila siku jaribu kufanya kitu kipya na cha tofauti kabisa na ulivyozoea kufanya.
Na kila unapoimaliza siku yako, jiulize yapi ya tofauti tofauti umeyafanya kwenye siku hiyo.
Kama hakuna, basi jua umeipoteza siku hiyo, hivyo usikubali tena kupoteza siku inayofuata.

Uwe na wakati mwema, na maandalizi bora ya kesho, ukijua kabisa kipi kipya unakwenda kujaribu kesho.

Kocha.