“People do not decide their futures, they decide their habits and their habits decide their futures.” – F.M. Alexander

Huwa tunajiambia na kuamini kwamba sisi ndiyo waamuzi wa kesho yetu.
Lakini huo siyo uhalisia, siyo sisi ambao tunaamua kesho yetu, bali ni tabia zetu ndiyo zinaamua kesho hiyo.

Ukijijengea tabia ya kuandika kila siku, tabia hiyo inakujenga kuwa mwandishi.
Ukijijengea tabia ya kuweka akiba kabla hujafanya matumizi, tabia hiyo inakujengea uhuru wa kifedha.
Ukijijengea tabia ya kutumia zaidi ya kipato, tabia hiyo inakuweka kwenye madeni na umasikini mkubwa.

Hakuna ambacho kibatokea kwenye maisha yetu mara moja, kila kitu ni zao la tabia ambazo tunejijengea siku za nyuma.
Unapoimaliza siku hii ya leo, jiulize ni tabia zipi ulizonazo ambazo zimekupa matokeo unayopata sasa.
Na pia jiulize ni tabia gani unahitaji kujijengea ili ziifanye kesho yako kuwa bora zaidi.

Uwe na wakati mwema.
Kocha.